Lugha za Kihindi-Kiajemi
Lugha za Kihindi-Kiajemi ni kundi kubwa zaidi katika familia ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Zinajumuisha lugha za Kihindi-Kiarya na lugha za Kiajemi (Irani). Zinazungumzwa zaidi kwenye Bara Hindi na Nyanda za Juu za Iran. Hapo zamani zilitumiwa pia katika Asia ya Kati, mashariki mwa Bahari ya Kaspi .
Lugha za Kihindi-Kiarya
haririKuna karibu lugha 221 za Kihindi-Kiarya (Indic), zenye jumla ya wasemaji zaidi ya milioni 800.
- Kibengali (lugha rasmi nchini Bangladesh; lugha rasmi ya jimbo la Bengala Magharibi nchini Uhindi)
- Kimarathi (lugha rasmi ya jimbo la nchini Uhindi)
- Kihindustani (kwa umbo la Kiurdu: lugha rasmi nchini Pakistan; lugha rasmi ya kieneo nchini Uhindi pamoja na Kihindi, aina nyingine ya Kihindustani)
Lugha za Kiajemi (Kiirani)
haririKuna karibu lugha 86 za Kiajemi, zenye wasemaji kati ya milioni 150 hadi 200.
- Kiajemi (lugha rasmi nchini Iran; pia rasmi kwa jina la Dari nchini Afghanistan na kama Kitajiki huko Tajikistan)
- Kipashto (lugha rasmi nchini Afghanistan)
- Kikurdi (lugha rasmi katika eneo la Kurdistan nchini Iraq)
Kinuristani, Kibangani, na Kibadeshi
haririWasomi wengine huchukulia lugha za Kinuristani na Kibangani kama sehemu ya kikundi kidogo cha Kihindi-Kiarya, lakini wengine wanazichukulia kama vikundi viwili tofauti vya Kihindi-Kiajemi. Lugha ya Kibadeshi pia ni lugha ya Kihindi-Kiajemi isiyopangwa bado kimakundi.
Vyanzo
hariri- Cardona, George. "Indo-Iranian languages". Indo-Iranian languages. https://www.britannica.com/topic/Indo-Iranian-languages. Retrieved 27 August 2018.
- Indo-Iranian. Iliwekwa mnamo 27 Agosti 2018.
{{cite book}}
:|work=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)