Kiwelisi
Kiwelisi (kwa lugha hiyo: Cymraeg; kwa Kiingereza "Welsh") ni kati ya lugha ya Kiselti ya nchi ya Welisi jirani na Uingereza kwenye kisiwa cha Britania.
Idadi ya wasemaji hukadiriwa kuwa kati ya watu 500,000 na 750,000.
Leo hi ndiyo lugha ya Kiselti yenye wasemaji wengi. Katika Welisi ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza.
Kiwelisi kimejulikana kwa kuwa na majina marefu sana, kwa mfano Llanfairpwllgwyngyllgogerychwyrndrobwllllantysiliogogogoch (sauti ya jina hili lasikika hapa) ambalo ni jina la kituo cha reli kwenye kisiwa cha Anglesey.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiwelisi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |