Kodi (kutoka neno la Kihindi) ina maana mbili:

  1. ushuru unaodaiwa na serikali ya nchi (kwa Kiingereza: tax) na
  2. pango yaani pesa anazotozwa mtu anapopangishwa nyumba au ardhi (kwa Kiingereza: rent au lease).

Kodi (ushuru)

hariri

Kodi (ushuru) ni malipo ya lazima ya pesa au aina nyingine ya malipo yanayotozwa na taasisi ya serikali kwa mujibu wa sheria kutoka kwa mlipakodi (mtu binafsi au chombo kingine cha kisheria) ili kufadhili matumizi mbalimbali ya umma.

Aidha katika ukusanyaji wa kodi lazima kuwe na sheria mama ambayo ni katiba ya nchi kuweka kifungu (clause) kinachotoa mamlaka kwa bunge kutunga sheria mbalimbali za kodi ili kuwezesha serikali kusimamia gharama mbalimbali za uendeshaji wa shughuli zake.

Kupitia upande wa serikali mamlaka iliyopewa kusimamia ukusanyaji wa kodi; utekeleza ukusanyaji wa kodi kwa mujibu wa sheria na pale inapotokea kutoelewana katika tafsiri ya sheria wakati wa utekelezaji basi chombo kilichopewa mamlaka kwa mujibu wa katiba ambacho ni mahakama hupokea shauri la kodi na kuanza kutafsiri sawa na taratibu na kanuni za sheria husika.

Kushindwa kulipa, au kukimbia au kupinga kodi, ni kosa la jinai na serikali ndio inayokushitaki uadhibiwe kadiri ya sheria.

Kodi zinajumuisha kodi ya moja kwa moja na kodi isiyo ya moja kwa moja.

Kodi (pango)

hariri

Kodi ya kupanga nyumba au ardhi ni malipo yanayofanyika kutokana na mkataba ambao anayekodisha nyumba au ardhi na mpangaji wa ile nyumba au ardhi huafikiana.

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kodi kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.