Valletta

(Elekezwa kutoka La Valletta)

Valletta (pia: La Valetta, kwa Kimalta: il-belt "mji") ni mji mkuu wa Malta wenye wakazi 7,100. Mji ulijengwa kama mji-boma kwenye ncha ya rasi ndogo inayozungukwa na maji ya bahari pande tatu.

Kitovu cha kihistoria cha Valetta.
Valetta mnamo 1680 kwa macho ya ndege.

Historia

hariri

Valletta limepokea jina lake kwa heshima ya Jean de la Valette aliyekuwa mkuu wa Wanamisalaba wa chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu. Valette aliamuru kujengwa kwa mji huu baada ya uvamizi wa Waturuki waliojaribu kuteka Malta mwaka 1565. Waturuki hawakufaulu wakafukuzwa na Valette aliona haja ya kuwa na mji imara kabisa kama hao watataka kurudi. Hivyo mji mpya ulijengwa kuanzia mwaka 1566 kwenye ncha ya rasi yenye bandari asilia bora.

Mnamo mwaka 1700 Valetta ilikuwa mji wenye ukuta imara kushinda miji yote.

Mji una majengo mengi ya kihistoria hata ukaingizwa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia.

Idadi ya wakazi imepungua kwa sababu watu wengi walikwenda kujenga mashambani.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Valletta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.