Lambati wa Vence
Lambati wa Vence (jina la kiraia kwa Kifaransa: Lambert Pelloquin; Bauduen, 1084 - Vence, 26 Mei 1154) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa, tangu mwaka 1114. Kabla ya hapo alikuwa mmonaki huko Lerins tangu umri wa miaka 16[1].
Anakumbukwa kwa kusaidia maskini, aliowajengea hospitali ya kwanza mjini, na kwa kupenda kuishi kifukara[2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Saint-Lambert sur diocese-frejus-toulon.com (Kifaransa)
- Lambert de Vence sur le site de l'Aumônerie de la cathédrale de Vence (Kifaransa)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |