Lazaro Hrebeljanović (kwa Kiserbokroatia Лазар Хребељановић; 1329 hivi – 15 Juni 1389) alikuwa mtawala mkuu wa Serbia baada ya Dola la Serbia kusambaratika, akimiliki mabeseni ya mito Morava: Morava kuu, Morava magharibi na Morava kusini tangu mwaka 1373 hadi kifo chake vitani.

Lazaro alivyochorwa (Monasteri ya Ravanica, miaka ya 1380).

Kwa msaada wa Kanisa la Kiorthodoksi la Serbia alijaribu kufufua dola hilo, lakini watawala wengine wa taifa hilo hawakumkubali.

Hatimaye Lazaro aliuawa katika Mapigano ya Kosovo alipoongoza jeshi la Wakristo dhidi ya lile la Dola la Osmani, lililoongozwa na Sultani Murad I.

Wakristo walishinda, lakini walikufa kwa wingi, kiasi kwamba mwaka uliofuata mjane wa Lazaro alikubali himaya ya Waosmani.

Lazaro anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Juni.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.