Lia Walti
Lia Joëlle Wälti (alizaliwa 19 Aprili 1993)[1] ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Uswisi ambaye anacheza kama kiungo wa katika klabu ya Arsenal ya Ligi Kuu ya Wanawake(WSL) na timu ya taifa ya Uswisi. Ni nahodha wa timu ya taifa ya Uswisi na nahodha wa nne wa Arsenal. Pia alikuwa nahodha wa klabu yake ya awali ya Turbine Potsdam. Kabla ya kusajiliwa na Arsenal mnamo Julai 2018, alichezea klabu ya Nationalliga A YB Frauen kuanzia 2009 hadi 2013 na kwa klabu ya Bundesliga Turbine Potsdam kuanzia 2013 hadi 2018.
Amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Uswizi tangu Agosti 2011.[2] Akiwa mchezaji wa kimataifa kwa walio na umri chini ya miaka kumi na tisa, alicheza Mashindano ya Uropa ya 2009[3] na Kombe la Dunia la 2010 kwa walio na umri chini ya miaka ishirini.[4]
Marejeo
hariri- ↑ "List of Players – Switzerland" (PDF). FIFA. 30 Mei 2015. uk. 22. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-05-28. Iliwekwa mnamo 31 Mei 2015.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Profile in the Swiss Football Association's website
- ↑ French and Swiss advance to semis. UEFA
- ↑ Statistics in FIFA's website
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lia Walti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |