Bundesliga

Bundesliga ni jina la michezo ya hali ya juu katika nyanja za michezo mbalimbali katika Ujerumani na Austria. Bundesliga ina maana ya kutaja ligi kuu ya nchi nzima. Mpira wa miguu ni mchezo mashuhuri sana katika nchi hizo mbili. Na ndiyo maana mchezo wa mpira wa miguu unajulikana sana katika nchi hizo kwa jina la Bundesliga.

Picha inayoonyesha sehemu ya timu za mpira za mashindano ya Bundesliga.

Timu za mpira zinaingia katika Bundesliga kwa kuwa washindi katika moja kati ya ligi ndogo za nchini humo. Timu itakayoongoza katika msimu wa mashindano hayo inaitwa Meister. Meister ni neno la Kijerumani lenye maana ya bingwa au mshindi. Kisheria, msimu wa michezo ya mpira huwa na kawaida ya kuanza Juni katika mwaka uliopo hadi Juni mwaka unaofuatia.

Timu itakayoongoza itategemea na ushindi au pointi walizozipata wakati wa msimu huo. Msimu huo umegawanyika katika sehemu mbili. Katika kila sehemu, kila timu zitashindana dhidi ya mwenzake. Katika mambo ya mpira wa miguu, timu itakayoshinda itapata pointi tatu. Kama mchezo utaisha bila kupattikana mshindi, basi timu zote mbili zitapata pointi mojamoja.

Idadi ya timu ni 20

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Bundesliga kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.