Tandawala
(Elekezwa kutoka Lophotis)
Tandawala ni ndege wakubwa wa familia ya Otididae. Tandawala kaskazi mkubwa ni ndege mkubwa kabisa duniani ambaye anaweza kuruka angani. Ndege hawa wana shingo refu, miguu mirefu na vidole vikubwa. Wakati wa majira ya kuzaa madume wana manyoya ya kuvutia na hufanya mikogo ya kubembeleza jike. Wanatokea kanda kavu za Afrika, Ulaya na Asia. Hula mbegu, wadudu na mijusi na hutaga mayai 2-5 chini.
Spishi za Afrika
hariri- Afrotis afra, Tandawala Mweusi (Southern Black Korhaan)
- Afrotis afraoides, Tandawala Mabawa-meupe (Northern Black Korhaan au White-quilled Bustard)
- Ardeotis arabs, Tandawala Arabu (Arabian Bustard)
- Ardeotis kori, Tandawala Mkubwa (Kori Bustard)
- Chlamydotis undulata, Tandawala Kaba (Houbara Bustard)
- Eupodotis caerulescens, Tandawala Buluu (Blue Korhaan)
- Eupodotis humilis, Tandawal Mdogo (Little Brown Bustard)
- Eupodotis rueppellii, Tandawala wa Rüppell (Rüppell's Korhaan)
- Eupodotis senegalensis, Tandawala Tumbo-jeupe (White-bellied Bustard)
- Eupodotis vigorsii, Tandawala wa Karuu (Karoo Korhaan)
- Lissotis hartlaubii, Tandawala wa Hartlaub (Hartlaub's Bustard)
- Lissotis melanogaster, Tandawala Tumbo-jeusi (Black-bellied Bustard)
- Lophotis gindiana, Tandawala Kishungi-hudhurungi (Buff-crested Bustard)
- Lophotis ruficrista, Tandawala Kishungi-chekundu (Red-crested Bustard)
- Lophotis savilei, Tandawala wa Savile (Savile's Bustard)
- Neotis denhami, Tandawala Machaka (Denham’s or Stanley's Bustard)
- Neotis heuglinii, Tandawala wa Heuglin (Heuglin's Bustard)
- Neotis ludwigii, Tandawala wa Ludwig (Ludwig's Bustard)
- Neotis nuba, Tandawala Nubi (Nubian Bustard)
- Otis tarda, Tandawala Kaskazi Mkubwa (Great Bustard)
- Tetrax tetrax, Tandawala Kaskazi Mdogo (Little Bustard)
Spishi za mabara mengine
hariri- Ardeotis australis (Australian Bustard)
- Ardeotis nigriceps (Great Indian Bustard)
- Chlamydotis macqueenii (Macqueen's Bustard)
- Houbaropsis bengalensis (Bengal Florican)
- Sypheotides indicus (Lesser Florican)
Picha
hariri-
Tandawala mweusi
-
Tandawala bawa-jeupe
-
Tandawala Arabu
-
Tandawala mkubwa
-
Tandawala kaba
-
Tandawala buluu
-
Tandawala wa Rüppel
-
Tandawala tumbo-jeupe
-
Tandawala wa Karuu
-
Tandawala wa Hartlaub
-
Tandawala tumbo-jeusi
-
Tandawala kishungi-hudhurungi
-
Tandawala kishungi-chekundu
-
Tandawala machaka
-
Tandawala wa Ludwig
-
Tandawala kaskazi mkubwa
-
Tandawala kaskazi mdogo
-
Australian bustard
-
Great Indian bustard
-
Macqueen's bustard
-
Bengal florican
-
Lesser florican