Louis Martin (Bordeaux, Gironde, Ufaransa, 22 Agosti 1823 - Arnières-sur-Iton, Eure, Ufaransa, 29 Julai 1894) alikuwa mwanamume Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Mt. Louis Joseph Aloys Stanislaus Martin.
Zulia iliyotumika siku ya kutangazwa mtakatifu mwaka 2015.

Pamoja na mke wake, Marie-Azélie Guérin, alitangazwa na Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 19 Oktoba 2008, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 18 Oktoba 2015.

Ni maarufu hasa kutokana na mtoto wao wa tisa na wa mwisho, mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, O.C.D., bikira na mwalimu wa Kanisa, aliyeandika vizuri ajabu juu ya uadilifu wao.

Maandishi

hariri

Mwaka 2011 barua 216 za Zélie na 16 za Louis Martin zilitolewa kwa Kiingereza katika kitabu A Call to a Deeper Love: The Family Correspondence of the Parents of Saint Therese of the Child Jesus, 1863–1885 (ISBN 0818913215).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  • THERESIA WA MTOTO YESU, Ua la Upendo, Maisha ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Aliyoyaandika Yeye Mwenyewe – tafsiri ya J. J. Rwechungura – ed. Paulines Publications Africa – Nairobi 1992 – ISBN 9966-21-021-0
  • THEREZA OW’OMWANA YEZU – Akamuli k’engonzi, Oburora bw’Omutakatifu Thereza Ow’omwana Yezu Obwo Yayehandikire Wenene – tafsiri ya J. J. Rwechungura – ed. Marianum Press Kisubi – Kisubi 1960

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.