Lugha ya kuundwa

(Elekezwa kutoka Lugha iliyotengenezwa)

Lugha ya kuundwa (au lugha unde) ni lugha ambayo misamiati na sarufi zake zimetungwa na watu badala ya kukua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Kwa kawaida zinaundwa kwa ajili ya kuwasiliana kati ya watu sawasawa na lugha asilia. Nyingi zinatengenezwa ili kuwa lugha saidizi za kimataifa, lakini nyingine zinaundwa kwa ajili ya usiri au majaribio ya isimu au bila sababu fulani.

Lugha ya kuundwa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto.

Mara chache lugha ya kuundwa maana yake ni lugha za kompyuta au za kuandaa programu (angalia lugha asilia). Kwa sababu ya utata huo watu wengi, hasa Waesperanto, hawapendi kutumia neno lugha ya kuundwa, na badala yake wanasema lugha ya kupangwa. Msemo lugha ya kupangwa unatumika kwa lugha zile tu ambazo ziliundwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu, kama Kiesperanto. Mfano mwingine wa lugha ya kuundwa ni lugha ya sheng' inayozungumzwa nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana. Lugha hiyo Haina wazawa asilia mahali popote ila tu ilizuka miongoni mwa vijana Kwa kutaka kusitiri mazungumzo Yao. Hivi ni kuunga mkono wazo la hapo awali kwamba lugha unde Huwa Kwa Sababu za kusitiri mazungumzo au kuunda programu za kompyuta kama vile lugha iitwaya "binary language" ambayo hutumika katika vifaa vya kielektroniki Ili kuundia programu zake. Lugha hiyo ndio hueleweka na mashine za kielektroniki kama tarakilishi au kikokotoo.

Marejeo

hariri
  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004 "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha ya kuundwa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.