Mabwepande ni jina la kata ya Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 14134[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 25,460 waishio humo. [2].

Kata ya Mabwepande
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Kinondoni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 25,460

Mabwepande ina msitu mkubwa ambao unaitwa msitu wa Pande. Msitu huu unajulikana kwa vitendo vya kigaidi ambapo Dr. Ulimboka alifanyiwa vitendo vya kigaidi katika msitu huo.

Ndani ya Mwabepande kuna mji mpya uitwao Kinondo unaokuja kwa kasi, ila wakazi wake wanalalamikia kutokuwa na daraja.

Kipindi cha mvua, Kinondo inageuka kuwa kisiwa, hivyo watoto wanashindwa kuenda shule. Pia mitaa mingine ambayo inapatikana Mabwepande ni Manzese, Banana, Monduli, Malolo, Mji mpya, Vikawe na Njechele.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewahi kufika katika kata hiyo kutatua migogoro ya ardhi.[3]

Historia ya Mabwepande hariri

Inasadikika kuwa hapo zamani Mabwepande ilikuwa ikiiitwa Mawepande kwa sababu kulikuwa na mawe makubwa mawili na msitu wa Pande, lakini ujio wa Wazungu ulibadilisha jina hilo kwa sababu walikuwa hawawezi kulitamka vizuri na kupelekea kuitwa Mabwepande.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Kinondoni - Tanzania  

BunjuHananasifKaweKigogoKijitonyamaKinondoniKunduchiMabwepandeMagomeniMakongoMakumbushoMbezi JuuMbweniMikocheniMsasaniMwananyamalaMzimuniNdugumbiTandaleWazo