Imamu

(Elekezwa kutoka Maimamu)

Imamu (kutoka Kiarabu: إمام‎ imām) ni istilahi ya Kiarabu yenye maana mbalimbali. Mara nyingi inamtaja kiongozi wa Kiislam, kama kiongozi wa msikiti au wa jamii. Maana ya msingi ni yule anayetoa mwongozo akistahili kufuatwa; kwa maana isiyo ya kidini neno hili linaweza kutaja pia timazi au kamba inayotumiwa kuelekeza mwendo wa matofali wakati wa kujenga nyumba au ukuta.[1]

Imamu akiongoza swala huko Kairo, Misri, mnamo 1865. Taswira ya Jean-Léon Gérôme.

Imamu anaitwa yule anayeongoza sala wakati wa swala ya Kiislamu.

Wasunni Edit

Kati ya Wasunni istilahi hilo linatumiwa kumtaja mtaalamu wa kidini, mara nyingi kama cheo cha heshima kwa waanzilishi wa madhab nne za Wasunni yaani Hanafi, Maliki, Shafi'i na Hanbali.[2]

Washia Edit

Kati ya Waislamu Washia "imamu" ni hasa yule kiongozi mmoja wa waumini anayetoka katika familia ya Mtume Mohammed. Kwa Washia Waismaili imamu ndiye Aga Khan. Kwa Washia Waithnashara maimamu ni hasa wafuasi 12 wa Muhammad kuanzia Ali ibn Abu Talib na watoto pamoja na wajukuu wake hadi Muhammad ibn al-Hassan anayeaminiwa kuwa imamu wa sasa aliyeingia katika hali ya kujificha wakisubiri kurudi kwake atakapoonekana tena[3] .

Huko Iran pia Ruhollah Khomeini anaitwa "imamu" (kwa matamshi yao "emam")

Marejeo Edit

  1. [https://archive.org/details/LANESARABICENGLISHLEXICONDIGITIZEDTEXTVERSION Lane, Edward William: Arabic – English Lexicon], Perseus Collection Arabic Materials, Attribution-ShareAlike 3.0 United States - CREATIVE COMMONS, Online Version, Released Digitized Text Version v1.1, Kitabu cha kwanza uk. 90-92
  2. Rabb, Intisar A. (2009). "Fiqh". In John L. Esposito. The Oxford Encyclopedia of the Islamic World. Oxford: Oxford University Press. doi:10.1093/acref/9780195305135.001.0001 . ISBN 9780195305135 .
  3. Virani, Shafique. "Khayrkhvāh-i Harātī" (in en). Encyclopaedia of Islam. https://www.academia.edu/43664942.

Tovuti za nje Edit