Majadiliano:Tanzania

Latest comment: miezi 5 iliyopita by Riccardo Riccioni in topic Twiga masai

Yah: Orodha ya mikoa. Sijui nani ameweka sanduku lenye majina ya mikoa. Mimi sina uhakika jinsi kuisahihisha. kwa sasa zote ni "Mkow wa..." . Ningeona afadhali kama ni: Arusha, mkoa wa; Mbeya, Mkoa wa... nakadhalika . Je mnaonaje? --Kipala 15:49, 25 Desemba 2005 (UTC)Reply

Kiswahili

hariri

Mwenzetu "196.41.57.3" alibadilisha sentensi juu ya lugha ya Kiswahili. Naona haifai kwa sababu Kiswahili ni lugha ya Kibantu. Na hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.

Ni kweli ya kwamba Kiswahili kimepokea maneno mengi kutoka lugha nyingi - hasa Kiarabu na Kiingereza - lakini hiyo haibadilihsa tabia yake. Vivyo hivyo Kiingereza ni lugha ya Kigermanik ingawa imepokea takriban 40% ya maneno yake kutoka lugha nyingine hasa Kifaransa ambacho ni lugha ya Kirumi.

Sentensi iliyobadilika inasema sasa ya kwamba Kiswahili ni lugha ya Kiarabu (na kadhalika). Hii si kweli. BAdo ni lugha ya Kibantu. Kwa sababu hiyo nitarudisha lugha ya awali. --Kipala 21:29, 25 Julai 2006 (UTC)Reply

Kikhoisan

hariri

Nimerudisha haliy a awali kuhusu makabila yenye lugha za Kikhoisan. Hawa ni Wasandawe na Wahadzabe lakini si Burunge. Linganisha makala ya Kiburunge na makala ya Ethnologue juu ya Wahadzabe.--Kipala 15:34, 11 Novemba 2007 (UTC)Reply

Makabila ya Tanzania

hariri

Kuna kitu sijaelewa pale. Kuna makabila mengine yametajwa, lakini madogo mno kuliko makabila yasiyotajwa halafu makubwa mno. Katika angalia yangu, nimeona makabila mengi yaliyotajwa mule ni ya huko bara na sio pwani. Makabila ya pwani hamna hata moja. Je, inasaidia nini ikiwa unataja makabila ya bara bila kutaja na hayo ya pwani?--Mwanaharakati (Longa) 13:50, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply

Sijui kama itasaidia nimeweka kiungo cha wazi kwa orodha ya makabila. Halafu nimetoa sentensi moja ambako fulani ameongeza makabila kadhaa hovyo; wanaotajwa sasa ni ama kulingana na ukubwa au kulingana na familia za lugha. Unaonaje? Menginevyo ni wikipedia hapa - mwandishi ni wewe!--Kipala (majadiliano) 14:40, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply
Tazama hii: Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma na Wanyamwezi, Wahehe na Wabena, Wagogo, Wahaya, Wamakonde, Wachaga, Waha na Wanyakyusa. Haya, kuna hawa watu wa Tanga, yaani makabila ya Tanga. Wazigua, Wadigo, Wabondei, n.k. wote hawajatajwa ilhali nao ni wengi. Hawa Wahehe, sizani kama wanafikia wingi wa kabila la Wazaramo. Hapa katika kutaja makabila haya ni bora kuw na marejeo ya maelezo hayo, yaani uthibitisho wa kuwa makabila hayo yana wingi huo. Vinginevyo ni bora kuonyesha ukurasa wa makabila yote bila kutaja idadi ya wafulani. Hapo vipi?--Mwanaharakati (Longa) 15:29, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply
Ukiwa na namba badilisha. en:Zaramo inasema idada ya Wazaramo ni 656,730 mwaka 2000, en:Wahehe 750,000 mwaka 1994. Chanzo cha namba katika wikipedia ni [1]. Nikichungulia orodha hii kuna watu wafuatao tu wanaotajwa kuwa na zaidi ya milioni: Wagogo, Waha, Wahaya, Wamakonde, Wanyamwezi, Wasukuma. Lazima kuongeza Wachagga ambao hawaorodheshwi na Enthnologue wka jina hili lakini kama vikundi (Machame n.k.). Wahehe - inawezekana kwa sababu namba ni ya 1994 na idadi inaweza labda kufikia milioni. Wote wengine - hapana. Nasahihisha ipasavyo. --Kipala (majadiliano) 16:42, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply
Ahsante kwa sahihisho lako. Haya, lakini hapa naona jengine. Ni kweli Tanzania kuna idadi ya watu wanaofuata dini za jadi na kufikia kiwango cha asiliamia 14?--Mwanaharakati (Longa) 16:53, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply
Dini - sijui. Sidhani ya kwamba mtu yeyote anajua. Kwa muda mrefu walisema theluthi Wakristo, Waislamu na imani za jadi. Lakini hii ilikuwa siasa tu. Hali halisi??? --Kipala (majadiliano) 17:13, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply
Maneno hayo!! Hata mie sijui, labda niseme kama unavyosema!! Siku imepita --Mwanaharakati (Longa) 17:21, 10 Desemba 2008 (UTC)Reply

Question about geographical names

hariri

Can anyone translate to Swahili geographical names listed below? Aotearoa (majadiliano) 08:30, 16 Novemba 2009 (UTC)Reply

  • Zanzibar Channel (strait)
  • Maasai Steppe; Masai Steppe
  • Arusha National Park > Hifadhi ya Taifa ya Arusha
  • Kilimanjaro National Park > Hifadhi ya Taifa ya (Mlima) Kilimanjaro

Twiga masai

hariri

Habari. Picha ya twiga imeandikwa Twiga masai, hii ni sahihi? Sijawahi kusikia kitu kama hicho. Asante FurahaKamili3 (majadiliano) 14:33, 30 Juni 2024 (UTC)Reply

Hata mimi sijasikia, ila sina hakika kama ni sahihi au siyo. Ukipenda, futa neno masai. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:07, 5 Julai 2024 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Tanzania ".