Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kipala (majadiliano) 08:03, 4 Aprili 2015 (UTC)Reply

Bwana Enock John Salamu! Asante kwa michango yako. Naomba uangalie Majadiliano:Mbute na ueleze kile unachofahamu kuhusu nililoweka huko. Kipala (majadiliano) 10:39, 5 Aprili 2015 (UTC)Reply

Salamu! Nadhani wewe ni mwanafunzi wa Jordan: au siyo? Swali moja: umefuta picha za Dar kwa makusudi au ni bahati mbaya? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:50, 7 Aprili 2015 (UTC)Reply
Habari! ndugu Riccardo, mimi ndie nimeweka hizo picha nilizozifuta haziendani na historia ya dar es salaam zinahusu timu ya mpira wa miguu ya yanga kwahiyo nimezitoa kwa sababu hiyo. Asante!Enock John (majadiliano) 09:06, 7 Aprili 2015 (UTC)Reply
Picha hizo zilikuwemo ndani ya makala hiyo kwa miaka zaidi ya mitano zikionyesha sehemu mbalimbali za Dar. Kwa hiyo nimezirudisha tena. Asante, --Baba Tabita (majadiliano) 03:59, 18 Aprili 2015 (UTC)Reply

Hii si kamusi sahili hariri

John salaam. Wikipedia hii ni kamusi elezo, si kamusi sahili. Wachangiaji wanaulizwa kuandika makala kuhusu mada ya kichwa, siyo kuweka maana ya maneno tu kama umefanya katika Mzee. Ukitaka unaweza kuchangia Swahili Wiktionary. ChriKo (majadiliano) 18:49, 14 Aprili 2015 (UTC)Reply

Ndugu Enock, ni kweli alichosema ChriKo. Tuna makala fupi na ndefu lakini pia makala fupi ni vema kukusanya habari kadhaa za kimsingi. Maana kamusi elezo inahitaji kiwango cha maelezo. Nimepanusha sasa makala ya Mzee. Labda ufuate ushauri wa Chriko, unaweza kuweka sentensi yako ya kiasili huko Swahili Wiktionary (kama haiko bado). Meginevyo ukitaka kuanzisha makala nashauri utazame makala inayolingana katika enwiki au simplewiki na chota mawazo huko. Hata kiona makala pale ni ndefu mno si kitu. Inatosha kuchukua habari za msingi na sentensi 2,3 zenye habari zinatosha kwa kuanzisha makala itakayopanuliwa baadaye.
Kuhusu mzee, ungeweza kuongeza maelezo kadhaa kwa mfano kuhusu "mzee wa kanisa", tofauti kati ya mzee wa kike na kiume, au mzee katika jamii / kabila fulani.

Kipala (majadiliano) 06:56, 15 Aprili 2015 (UTC)Reply

asante nimejifunza mambo mengi kupitia jinsi ulivyo kuza kuhusu neno Mzee na namna ya kuongeza maneno mengine kuhusu mada husika.Enock John (majadiliano) 08:48, 19 Aprili 2015 (UTC)Reply

Qadosh na Agios hariri

Ndugu, maneno hayo mawili yanatafsiriwa kwa kawaida "mtakatifu" (holy), ingawa kuna tofauti ndogondogo kati ya lugha moja na nyingine (kama kawaida). Niseme kwamba neno la Kiebrania קדוש linazingatia upekee wa Mungu unaomtofautisha na vitu vyote kuliko usafi wake wa kimaadili. Endelea kusoma Biblia! Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:01, 7 Mei 2018 (UTC)Reply

Majadiliano hariri

Habari zako bwana Enock john.naomba unipe mwongozo zaidi kuhusu kuandika makala pamoja na kujua kamusi hii ya kiswahili, pia jinsi ya kuandika anwani ya kupokea kuki

jinsi ya kuandika anwani hariri

Habari ndugu. Asante kwa swali lako, kuhusu kuandika anwani unatakiwa unapo maliza kuandika malizia na Alama za utambulisho wako ambazo ni sangija (majadiliano) 10:17, 15 Machi 2019 (UTC) ziwe mwisho wa ujumbe wakosangija (majadiliano) 10:17, 15 Machi 2019 (UTC)Reply

jinsi ya kuandika anwani hariri

Habari ndugu. Asante kwa swali lako, kuhusu kuandika anwani unatakiwa unapo maliza kuandika malizia na Alama za utambulisho wako ambazo ni sangija (majadiliano) 10:10, 15 Machi 2019 (UTC) ziwe mwisho wa ujumbe wakosangija (majadiliano) 10:10, 15 Machi 2019 (UTC)Reply