Magret Hamisi hariri

Salam, Ndugu Hadj. Kwa karibu sana katika Wikipedia kwa Kiswahili! Nimeona machache uliyoandika kuhusiana na waigizaji kadhaa wa filamu wa nchini Tanzania. Lakini bado haujaweka ile kitu ya kuitwa Notability, yaani UMAARUFU. Kama inawezekana mwekee filamu alizoigiza na kuona yeye maarufu. Mengineyo nimeona ukiandika bila kuweka CATEGORY. Category au JAMII ni muhimu sana kuweka wakati wa kumaliza kuandika makala zako. Unachotakiwa kufanya ni kuweka:

  • [[Category:Waigizaji Filamu wa Tanzania]]

Basi hapo kila kitu kitakuwa sawa!! Kuhusu kutumia zana hizi, bado utahitaji uzoefu wa siku mbili-tatu! Karibu sana, niite Muddyb Blast au,--Mwanaharakati (majadiliano) 12:21, 11 Septemba 2008 (UTC)Reply

Muundo wa makala za Wikipedia hariri

Labda nikupe tena machache kuhusiana na muundo na namna ya kuandika makala katika Wikipedia hii. Nimeona ukiandika:

Anne Mwampamba Miaka yake ni 34, Elimu ya sekondari Meta, Mbeya Ni Mkristo, Mfanyakazi wa kampuni ya City Elevator ya Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ni muigizaji wa kikundi cha sanaa cha Alwatan kinachotngeneza filamu za kibongo nchini Tanzania.

Hizo sio kanuni na taratibu za uumbaji wa makala za Wikipedia. Labda fuata mwelekeo huu ambao mara nyingi unafanywa na wachangiaji wa Wikipedia!

Anne Mwampamba (amezaliwa 25 Juni, 1974) ni mwigizaji wa filamu na tamthilia kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa kucheza katika filamu...... Pia ni mmoja kati ya wanakundi la maigizo maarufu kama Alwatan... Anne ni mwigizaji na pia mfanyakazi wa kampuni moja iitwayo City Elevator ya mjini Dar es Salaam, Tanzania. Anne pia ni mama wa mtoto mmoja aitwaye....

Natumai utakuwa umenipata vilivyo! Basi tuendelee.--Mwanaharakati (majadiliano) 12:43, 11 Septemba 2008 (UTC)Reply

Samahani sana Nd. Hadji. Nimeona kila nikituma ujumbe kwako naona haujibiwa kabisaa! Na ndiyomaana nimeamua kukuzuia kwa muda kadhaa. Hutoweza kuhariri Wikipedia hii hadi utakapo soma maelezo yote ya juu kisha utueleze kama umeelewa? Ili uweze kuhariri kama awali, basi nitumie e-mail kupita:

Mara moja nitaupata! Halafu usijisikie vibaya kwa kuwa umefanyiwa hivyo, ni katika kukutaka upate kuelewa ni nini unachokifanya! Kwa sasa, bado hujajua ni nini unachofanya (samahani), ila unatakiwa ujue ni nini cha kufanya.Karibu sana.--Mwanaharakati (majadiliano) 13:04, 11 Septemba 2008 (UTC)Reply

Yupo? hariri

Nimefuta leo makala ya "uandishi wa habari" iliyoandikwa na Hadj. Yaliyomo ya makala hayakulingana na kichwa hata kidogo. Sijui kama Bwana Hadj anasoma ukurasa wake hapa. Ukisoma naomba jibu kwa sababu tukifurahia michango kuna utaratibu wake jinsi alivyoeleza Muddy. Naona heri tuwasiliane wazi. --Kipala (majadiliano) 08:43, 12 Septemba 2008 (UTC)Reply

Your account will be renamed hariri

08:28, 20 Machi 2015 (UTC)

Renamed hariri

11:57, 19 Aprili 2015 (UTC)