Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Anuary Rajabu (majadiliano) 11:17, 21 Aprili 2023 (UTC)Reply

Ndugu, imenibidi kukuzuia, kwa sababu unaingiza taarifa zisizo na hakika, sanasana ni maoni yako. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:06, 21 Aprili 2023 (UTC)Reply
Samahani ndugu. Lakini hujafanya jambo jema. Ingefaa kama ungetoa katazo kwanza, kabla hujachukua uamuzi huo. Hiyanius Srenius (majadiliano) 16:24, 21 Aprili 2023 (UTC)Reply
Ndugu, shida ni kwamba michango mingi mibovu inamaliza muda wetu. Tunalazimika kuifuta ua kuirekebisha badala ya kutunga makala mya zenye ubora. Basi, nitaondoa zuio, mradi una nia ya kuwa makini zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:39, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply
Ndugu, nimekuzuia tena kwa sababu unazidi kuingiza taarifa zisizokubalika sana, kwa mfano kwamba Warombo si Wachagga. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:45, 28 Aprili 2023 (UTC)Reply
Ni kweli mimi mwenyewe mrombo. Na nilichokiandika ni kweli. Hiyanius Srenius (majadiliano) 20:23, 28 Aprili 2023 (UTC)Reply
Nilikwishaelewa kwamba wewe ni Mrombo, lakini wanaosema kuwa nyinyi si Wachagga ni wachache mno. Sehemu nyingine, kama nimeelewa vizuri, uliandika Wapare ni Wachagga. Au siyo? Unapoandika kitu lazima kiwe kinakubalika, la sivyo uandike kwamba ni maoni ya wachache na utoe hoja zao kama hoja, si jambo la hakika kwa sababu tu wewe unaziunga mkono! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:44, 29 Aprili 2023 (UTC)Reply

Habari kaka Riccardo Riccioni hariri

Je kama mtu ameweka mada kwenye wikipedia na marejeo mbalimbali huwa kuna malipo yoyote analipwa? Hiyanius Srenius (majadiliano) 14:51, 30 Aprili 2023 (UTC)Reply

Hakuna kabisa. Lengo la Wikipedia ni kueneza ujuzi bure. Sanasana kuna mashindano yenye tuzo fulani katika nafasi maalumu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:54, 1 Mei 2023 (UTC)Reply

KUZUILIWA AKAUNTI MARA KWA MARA NINAHARIRI hariri

Nimekuwa nikizuiwa Mara Kwa mara Tatizo Nini na nifanye Nini? Hiyanius Srenius (majadiliano) 15:34, 12 Mei 2023 (UTC)Reply

Afadhali umwandikie moja kwa moja aliyekuzuia. Fungua ukurasa wake wa majadiliano, piga "hariri chanzo", kopi kichwa hapo juu pamoja na swali lako na hifadhi mabadiliko. Kipala (majadiliano) 16:33, 12 Mei 2023 (UTC)Reply
Ndugu, michango yako haikidhi kiwango cha kamusi elezo kama hii. Wewe unaandika maoni yako kama katika mitandao ya jamii, bila kujali kama yanakubalika au siyo wala kuweka vyanzo vya taarifa zako. Unatunga makala fupi za mstari moja, bila kuangalia sana tofauti za herufi kubwa na ndogo, n.k. Sijakuzuia milele, ila kwa wiki tu, ili ujipange vizuri zaidi. Angalia kurasa zetu zilivyo, ili kwanza ujifunze namna ya kuchangia kwa tija. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:36, 13 Mei 2023 (UTC)Reply
Ndugu, unaendelea kupotosha habari kuhusu Wachaga. Nani atakubali kwamba Wapare ni Wachaga na Warombo sio? Halafu hawa Waseri, habari zao unaziota usiku? Taja chanzo chochote cha kuaminika! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:13, 1 Oktoba 2023 (UTC)Reply

Muundo wa Makala hariri

Habari ndugu,

Uhali gani? natumaini ubuheri wa afya tele. Nimepitia hariri zako na majadiliano yako kwenye ukurusa wako huu wa mtumiaji umeonywa sana kuhuhusu uhariri wako. Je, bado hujajifunza kitu kuwa ni wapi unakosea?

Leo pia nimepitia baadhi ya makala ulizohariri na kuanzisha bado makosa yanajirudia yaleyale, baadhi ya machapisho nimelazimika kuyafuta maoja kwa moja kwani ni mabiovu mnoo, na baadhi nimerekebisha muundo na mpangilio wa makala kw ujumla mfano huu ukurasa wa (Waseri), tafadhali jaribu pitia tena ukurasa huo na ujifunze kupitia mabadiliko yalifanyika kwenye makala hiyo.

Pia nimelazimika kukuzuia kuhariri kwa siku moja, kukupa nafasi ya kujifunza mpangilo na namna sahihi na stahiki ya uanzishaji na uhariri wa makala tafadhali nenda kwenye kiungo hiki ( Wikipedia Mwongozo ) kujifunza kujifunza kila kitu kuhusu kuhariri, kuanzisha makala, muundo n.k.

Amani kwako! Anuary Rajabu (majadiliano) 19:41, 13 Oktoba 2023 (UTC)Reply