Waseri ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro.lugha yao rasmi ni kiseri. Waseri wanajishugulisha na kilimo, ufugaji,biashara na kazi za ofisini. pia wanaweza kufanya kazi zingine za ufundi nk.Tofauti ya Waseri na wachaga ni kubwa sana hasa katika Lugha pamoja na mila na desturi,ikiwemo chakula chao cha asili na matambiko. Chakula cha asili cha waseri ni Kitheri,umberere,mabande,ngolowo,iromboe,ng'ande na Mtori. Hata hivyo kwa sasa Mtori unaliwa na watu mbalimbali ambao sio waseri na hupikwa mahotelini kama chakula.


Irombwe ni chakula cha asili cha waseri kinachopikwa kwa mahindi na maharage.

JINSI YA KUPIKA

Andaa mahindi,maharage,mafuta ya kula,chumvi, na jiko,unaweza kutumia jiko la gesi,jiko la mkaa, au jiko la umeme. Anza kuchambua mahindi yako na maharage vizuri,weka kwenye chombo Kisha osha mahindi na maharage. Baada ya kuosha tafuta sufuria safi weka mahindi yako kwenye sufuria kisha washa jiko lako. Weka maji kwenye sufuria yenye mahindi Kisha weka sufuria Yako kwenye moto tayari kuanza kupika. Acha mahindi yako yaendelee kuiva Kwa saa kadhaa. Mahindi yakikaribia kuiva weka maharage. Alafu subiri tena kwa saa kadhaa. Maharage yakishaiva weka chumvi na mafuta ya kula kisha anza kusonga mchanganyiko wa mahindi na maharage mpaka uchanganyike vizuri.baada ya kuhakikisha umesonga mchanganyiko na kuchanganyika vizuri epua irombwe yako weka kwenye sahani safi tayari kwa kuliwa.


Tofauti nyingine ya wachaga na waseri ipo kwenye kinywaji chao cha asili.inafahamika kuwa wachaga wana pombe yao inayoitwa mbege. Lakini warombo wao ni tofauti kabisa,wao wana kinywaji chao ambacho kinaitwa busa. Utengenezaji wa busa na mbege ni tofauti kabisa kwani busa ni tamu zaidi. pia waseri hunywa busa kipindi wakifanya matambiko mbalimbali, kwani ni kinywaji mahususi kinachotayarishwa Ili kitumike wakati wa tambiko. Matambiko ya waseri hufanyika wakati wowote katika mwaka,pia hufanyika kwa lengo la kuiomba mizimu ya kilimanjaro iwasaidie katika mambo mbalimbali. tambiko hufanyika katika mti maalumu,ulioandaliwa kwaajili ya tambiko. miti hii huoteshwa katika kila kaya kwaajili ya kutunza mazingira na chakula cha mifugo. waseri wameenea mkoa wote wa kilimanjaro hutambuana kwa kuelewana katika mazungumzo .Itambulike kuwa waseri sio wachaga, kwani lahaja yao ni tofauti kabisa na lahaja ya kabila la wachaga, ambalo ndilo kabila kubwa katika mkoa wa Kilimanjaro. Lahaja ya lugha ya kichaga imeandikwa vizuri katika kitabu cha "A course in the vunjo dialect of the kichagga language of kilimanjaro Tanzania" kilichoandikwa na Bernard Leeman, Lahaja hii ndicho kichagga halisi ambayo inafanana sana na ile lahaja ya wapare,mwika,kiruavunjo,kilema,marangu,marangumamba,kibosho,siha,uru,machame na meru. Ambayo ni tofauti sana na lahaja ya lugha ya  kiseri ya kabila la waseri


Unaweza pia kusoma.

Moshi




REFFERENCE

[1][2]

[3]


[4]

  1. Lugha za Kibantu
  2. Nyabola, Nanjala (2022-10-13). "Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia". foresight. ISSN 1463-6689. doi:10.1108/fs-11-2021-0222. 
  3. Martin, Malin D. (1957-07). "Cleidocranial Dysostosis: Two Cases". The Guthrie Journal 27 (1): 5–13. ISSN 0882-696X. doi:10.3138/guthrie.27.1.005.  Check date values in: |date= (help)
  4. Buberwa, Adventina (2023-03-23). "Changamoto katika matumizi ya majina ya lugha za kigeni nchini Tanzania: Mtazamo wa Nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu". Kioo cha Lugha 20 (1): 115–129. ISSN 0856-552X. doi:10.4314/kcl.v20i1.8.