Innocent Cosmas Msoka
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Kupitia masahihisho
haririNdugu, hongera kwa juhudi zako. Maendeleo yapo, ila naomba upitie mabadiliko ya makala zako kwa sababu unarudiarudia makosa yaleyale nami nalazimika kurudiarudia masahihisho yaleyale. Ningekuwa na muda zaidi ningeboresha zaidi lakini naishia kufanya yaliyo muhimu zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:03, 17 Oktoba 2024 (UTC)
- Ndugu, naomba katika jamii ya hao wanabaiskeli wa Italia, badala ya jamii:wanamichezo wa Italia, sasa tuandike jamii:waendeshabaiskeli wa Italia kwa sababu wamekuwa wengi mno na bado mnawaongeza. Hongera na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:15, 27 Oktoba 2024 (UTC)
- Sawa sawa Nitarekebisha hilo, Ahsante sana kwa Hongera na Hongera na Ahsante sana kwa maelekezo naahidi kuzingatia hilo! Amani iwe kwako pia! 41.89.10.241 13:24, 27 Oktoba 2024 (UTC)
- Salamu Cosmas,Tafadhali pitia maandiko yako, bado kuna makosa ya tafsiri yanayotokea, na makosa hayo yanaharibu maana katika tafsiri sanifu ya KIswahili,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 14:19, 30 Oktoba 2024 (UTC)
- Sawa sawa Nitarekebisha hilo, Ahsante sana kwa Hongera na Hongera na Ahsante sana kwa maelekezo naahidi kuzingatia hilo! Amani iwe kwako pia! 41.89.10.241 13:24, 27 Oktoba 2024 (UTC)
Habari ndugu @Innocent Cosmas Msoka nakukumbusha kuendelea kupitia masahihisho ya makala zako yanayo fanywa na wahariri wengine ili kuepuka kurudia makosa yaleyale. Wakabidhi hatuna mda mrefu wa kupitia makala hizi. Amani kwako Justine Msechu (majadiliano) 14:08, 31 Oktoba 2024 (UTC)
- Ndugu, bado hujapata desturi ya kupitia masahihisho yetu ili usirudie makosa yaleyale na kusababisha tupoteze muda mwingi. Tafadhali, angalia. Kwa mfano, mwanzoni mwa makala ndani ya mabano tunaweka taarifa fupi tu kuhusu kuzaliwa na kufariki. Kama mtu hajafariki, tunaandika "amezaliwa", lakini kama amekufa, inaeleweka kuwa tarehe ya kwanza ni ya kuzaliwa na ya pili na ya kufariki. Pia katika haraka, mara mbili ulirudia kuchapa ukurasa uleule mmoja kwa watu wawili tofauti, ndiyo sababu nilipaswa kufuta zile zilizokosewa. Pamoja na hayo, hongera kwa juhudi zako! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:01, 2 Desemba 2024 (UTC)
- Asante sana, Ndugu Riccardo, kwa kunielekeza na kwa uvumilivu wako. Naomba radhi kwa makosa niliyofanya na kwa usumbufu uliosababisha. Nitazingatia masahihisho yako kwa makini zaidi na kuhakikisha sipuuzi maelekezo yaliyotolewa.
- Nitajitahidi kupitia kazi yangu mara mbili kabla ya kuwasilisha ili kuepuka kurudia makosa kama hayo. Nashukuru pia kwa hongera zako na kwa msaada wako wa kunifanya niwe bora zaidi. Amani kwako pia! -- Cosmas Innocent Cosmas Msoka (majadiliano) 15:11, 2 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, umenijibu vizuri, lakini labda hujanielewa. Naomba urudie kusoma kwa makini niliyokuandikia jana. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:45, 3 Desemba 2024 (UTC)
- Hapana shaka, Ndugu. Nitarejea kusoma ujumbe wako wa jana kwa makini zaidi ili kuhakikisha ninakuelewa vema. Asante sana, na amani iwe nawe pia! ~2024-21645 (talk) 10:47, 3 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, pamoja na majibu yako mazuri, unaendelea kwenda haraka kutunga kurasa zenye makosa yaleyale...
- Pia uelewe kigezo {{BD}}. Ni hivi: {{BD|Mwaka wa kuzaliwa, yaani, 1958|usiweke kitu - ila kama mtu kafa weka mwaka aliokufa, yaani, 2009}}
- Hapana shaka, Ndugu. Nitarejea kusoma ujumbe wako wa jana kwa makini zaidi ili kuhakikisha ninakuelewa vema. Asante sana, na amani iwe nawe pia! ~2024-21645 (talk) 10:47, 3 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, umenijibu vizuri, lakini labda hujanielewa. Naomba urudie kusoma kwa makini niliyokuandikia jana. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:45, 3 Desemba 2024 (UTC)
- Chumba cha kwanza mwaka wa kuzaliwa tu
- Chumba cha pili mwaka aliokufa
- ANGALIZO
- Usiweke jamii yoyote kama vile: "waliozaliwa", "waliofariki", na "watu walio hai". Ukiweka {{BD|1950|}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "watu walio hai".
- {{BD|1950|2012}} - katika jamii itataja "waliozaliwa 1950" na "waliofariki 2012".
- Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:32, 5 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, ndugu, tafadhali, legeza mwendo ili ujifunze vizuri zaidi. Mbona huangalii ninavyopoteza saa nyingi kusahihisha makala zako? Tafsiri unazotumia mara nyingine ni kichekesho kabisa. Nini maana ya "mbio za Kiitaliano" au "Mtaliano wa zamani" au "wa barabara na wimbo"? "Wa Kiitaliano" maana yake ni lugha anayotumia, si uraia wake. Ukiendelea na makosa yaleyale itanibidi kukusimamisha kidogo kwanza. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:08, 10 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu Riccardo,
- Asante kwa maoni yako yenye manufaa na kusisitiza umuhimu wa kufafanua maneno vyema ili kuepusha mkanganyiko. Nimeyasoma kwa makini maelezo yako na nakubaliana kwamba kuna maeneo yanayohitaji maboresho katika tafsiri zangu.
- Nitachukua hatua madhubuti kuhakikisha kwamba matumizi ya lugha na tafsiri ni sahihi zaidi, hasa inapohusisha dhana kama uraia, lugha, na muktadha wa neno. Nitalenga kuelewa vizuri zaidi maelezo yako na kuzingatia ushauri wako ili kupunguza kazi ya kusahihisha unayolazimika kufanya.
- Naomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza. Nitafanya jitihada zaidi ili kuhakikisha ubora wa kazi zangu unaimarika. Amani iwe nawe pia!
- Cosmas Innocent Cosmas Msoka (majadiliano) 19:17, 10 Desemba 2024 (UTC)
- Mpendwa Riccardo Riccioni,
- Natumai ujumbe huu utakufikia ukiwa salama na mwenye amani.
- Ninakuandikia kwa unyenyekevu mkubwa kuomba msamaha kuhusiana na hatua ya kunizuilia kuhariri makala kwenye Wikipedia. Kwa dhati kabisa, ningependa kueleza kuwa mimi ni mhariri wa kujitolea ambaye huchangia kwa upendo mkubwa katika jukwaa hili muhimu. Kujitolea kwangu kwa Wikipedia ni sehemu ya juhudi zangu za kushirikiana katika kueneza elimu na maarifa kwa watu wengi.
- Hata hivyo, kizuizi hiki kimenivunja moyo sana na kunikosesha furaha, kwa kuwa napenda sana kuwa sehemu ya jumuiya hii. Kwa heshima na unyenyekevu, naomba kwa dhati kwamba unizingatie na kufikiria kuniondolea kizuizi hiki. Nia yangu ni kuendelea kuchangia kwa njia nzuri na yenye manufaa kwa jumuiya nzima ya Wikipedia.
- Ninaahidi kuheshimu na kufuata taratibu zote za jumuiya hii katika harakati za kufanya mabadiliko au kuhariri maudhui. Ikiwa kuna chochote unachohitaji kujadili nami kuhusu hali hii, niko tayari kushirikiana nawe kwa uwazi.
- Asante sana kwa muda wako na kwa kuchukua hatua ya kusikiliza ombi hili. Natarajia usaidizi wako wa kuniruhusu tena kuhariri makala.
- Amani Kwako,
- Innocent Cosmas Msoka
- (Mhariri wa Wikipedia wa kujitolea) Innocent Cosmas Msoka (majadiliano) 12:01, 12 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, ndugu, tafadhali, legeza mwendo ili ujifunze vizuri zaidi. Mbona huangalii ninavyopoteza saa nyingi kusahihisha makala zako? Tafsiri unazotumia mara nyingine ni kichekesho kabisa. Nini maana ya "mbio za Kiitaliano" au "Mtaliano wa zamani" au "wa barabara na wimbo"? "Wa Kiitaliano" maana yake ni lugha anayotumia, si uraia wake. Ukiendelea na makosa yaleyale itanibidi kukusimamisha kidogo kwanza. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:08, 10 Desemba 2024 (UTC)
@Riccardo Riccioni @Justine Msechu @CaliBen @Edward Jacobo @Hussein m mmbaga Innocent Cosmas Msoka (majadiliano) 12:03, 12 Desemba 2024 (UTC)
- Ndugu, hakuna anayekanusha nia njema na bidii zako. Shida umepitiliza. Harakaharaka haina baraka. Nilikuonya mara kadhaa uwe makini zaidi, lakini badala yake ukakaza mwendo. Mamia ya kurasa zinazohitaji marekebisho madogomadogo yananipotezea saa nyingi nisiweze kufanya kazi zangu. Hata hivyo nilikusimamisha kwa siku moja tu, hivyo kesho utaweza kuendelea. Ila naomba utumie saa zilizobaki kupitia masahihisho yangu, hata kama si yote. Itakusaidia sana kuboresha michango yako. Usivunjike moyo, uwe na amani. Tupo pamoja! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:48, 12 Desemba 2024 (UTC)
- @Riccardo Riccioni, Naomba radhi tena kwa kusababisha usumbufu na kazi ya ziada kutokana na harakati zangu za kuhariri. Nia yangu ilikuwa njema, lakini nakubali kuwa pengine kasi yangu ilipitiliza na ikaathiri kazi yako.
- Ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kurejea kesho, lakini kwa unyenyekevu, naomba ukiona inafaa, unaweza kuniondolea kizuizi leo kama itakupendeza? Ningependa kutumia muda huu kuanza kufanya marekebisho kwa mujibu wa mapendekezo yako.
- Najua umesema nichukue muda huu kusoma masahihisho yako, jambo ambalo nitazingatia, lakini ningefurahi pia kuanza kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo. Hii itasaidia pia kufanikisha marekebisho kwa wakati na kwa ufanisi zaidi.
- Naahidi kuchukua hatua kwa umakini zaidi siku zijazo na kufuata ushauri wako ili kuepuka hali kama hii tena. Asante sana kwa uvumilivu wako na mwongozo wako muhimu.
- Naomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na ninashukuru kwa msaada wako.
- Amani kwako,
- Innocent Cosmas Msoka
- (Mhariri wa Wikipedia wa kujitolea) Innocent Cosmas Msoka (majadiliano) 12:54, 12 Desemba 2024 (UTC)
- Hujaathiri kazi zake. Ila unampa kibarua kisicho na lazima. Soma maelezo, tuliza kichwa. Andika ama tazama kile alichokiandika kisha jifunze kupitia hayo. Sisi wengine tunafurahia mchango wa Riccardo kwa kutusahihisha. Punguza mwendo. Said Mfaume (majadiliano) 13:31, 12 Desemba 2024 (UTC)