Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Muddyb MwanaharakatiLonga 06:31, 25 Novemba 2009 (UTC)

ViungoEdit

Salaam Bwana Kamero naona kwa furaha makala ulizoweka ulichagua maada za maana! Naona tatizo 1 inayorudia mara nyingi ni viungo unavyoweka. Ukiingiza nukta au koma ndani ya mabano hutapata kiungo sahihi kamwe. Linganisha Wikipedia:Makosa#8_Kuvuruga_viungo_kwa_nukta_na_koma, pamoja na sehemu nyingine za orodha ile kuhusu viungo vipya na kazi ya kuchungulia makala zilizopo tayari. Jaribu kuangalia makala zako upya kufuatana na orodha lile la makosa pamoja na ushauri mwingine katika wikipedia:Mwongozo. --Kipala (majadiliano) 18:30, 12 Desemba 2009 (UTC)

Namimi ningezee hili. Ukitaka kutumia jamii au category, siyo lazima kuchukua yale yote kutoka Wikipedia ya Kiingereza! Kwa mfano makala ya Koffi_Olomide - nimeiwekea jamii na kusawazisha hasa mwanzoni mwa makala. Kuhusu jamii ya watu walio hai na hao waliofariki, basi tumia hizi: [[Jamii:Watu Walio Hai]] na [[Jamii:Walifariki...]] na [[Jamii:Waliozaliwa ....]]. Ukiwa una swali uliza tu!--  MwanaharakatiLonga 07:40, 15 Desemba 2009 (UTC)

MtamaEdit

Nimerejesha yale uliyoingiza chini ya mtama. Uliweka maandishi yako bila kuangalia makala iliyokuwepo tayari. Makala ilikuwa tayari na habari muhimu kuhusu uainishaji; yale uliyoweka haina maelezo ya aina hii. Nakuomba hakikisha ili usiandike tena juu ya makala iliyopo bila majadiliano ya awali. Uko huru kuongeza habari (ukihifadhi kwanza kazi yako ya translate.google penginepo) kwa mfano juu ya historia ya nafaka hii. --Kipala (majadiliano) 13:36, 15 Desemba 2009 (UTC)

Makosa ya NUKTA na KOMAEdit

Salaam, Kaka. Nimeona mara kadhaa unaweka KOMA na NUKTA ndani ya mabano mraba ya ya kioungo cha ndani (mfano [[Kenya,]] na [[Kenya.]]= matokeo Kenya, na Kenya.). Hii inaleta tokeo la uongo kabisaa. Inatakiwa iwe: [[Kenya]], na [[Kenya]]. = matokeo Kenya, na Kenya.

Tegemeo langu ni kwamba lazima utalielewa hili. Nimeona mara nyingi na kuna uwezekano mkubwa wa kupunguziwa maksi endapo tatizo hili litaendelea, kaka. Tuendelee.--MwanaharakatiLonga 15:22, 21 Desemba 2009 (UTC)

Ukitaka kujibu ujumbe huu, tafadhali fungua hapa na uanze kuandika maneno yako chini ya maandishi haya. Jaribu kwanza halafu mwisho wa maandishi yako weka alama ya --~~~~. Jaribu, kaka.--MwanaharakatiLonga 15:25, 21 Desemba 2009 (UTC)