Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 11:17, 3 Julai 2021 (UTC)Reply

Ndugu, usiondoe mabano ya mraba katika makala. Wenzako tumeyaweka kwa makusudi. Viungo vyekundu ni kichocheo cha kuandika makala mpya. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:33, 4 Julai 2021 (UTC)Reply

Umeacha kasorotafadhali upitilie makala zako zote angalia marejeo hariri

Habari asante kwa michango yako lakini kuna kasoro nzito hasa upande wa marejeo (footnotes / references)

  1. Zayn_Africa - hakuna marejeo yanayokubaliwa. Marejeo ya Wikipedia haikubaliwi. Sasa ni makala bila chanzo ambayo ni sababu ya kuifuta. Unaweza kuchagua katika Wikipedia ya Kiingereza na kuchukua marejeo yenyewe huko. Angalia hapa Wikipedia:Mwongozo_(Kutaja_vyanzo), sehemu kuhusu Marejeo tata!
  2. Makala mengine hujaweka chazo chochote. Hii ni pia sababu ya kufuta makala yako. (mfano Tyga, Sauti Sol)
  3. Naomba uthibitishe umesoma na kuelewa ninachoandika. Halafu nenda usahihishe, usiendelee kutunga makala mapya kabla ya kusahihisha! Kipala (majadiliano) 17:13, 4 Julai 2021 (UTC)Reply
Basi naona kasoro hazikuwa zako, uliongeza picha. asante. Ila ukiona makala yasiyo na marejeo au lugha isiyoeleweka, tafadhali uongeze juu ya makala alama za {{vyanzo}} au {{lugha}}. Au ingiza marejeo (tazama juu)Kipala (majadiliano) 21:06, 4 Julai 2021 (UTC)Reply
Ndugu, uwe makini zaidi: Kathy Keeton amegeukaje kuwa Kachi ketone? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:01, 30 Oktoba 2021 (UTC)Reply
sawa Mohamed mfuu (majadiliano) 15:29, 19 Machi 2022 (UTC)Reply

Jamii hariri

Ndugu umetunga makala za viwanja vya ndege na kuzipanga katika jamii za utalii. Hii si sahihi, naomba ufanye utafiti kabla kushughulika mada mpya. Kwanza si kila uwanja wa ndege unaohusika katika utalii, pili mahali pengi utalii -hata kama uko- si jambo muhimu sana ukilinganisha na uchumi mwingine; tatu tuna Jamii:Uwanja wa Ndege, pia kwa nchi mbalimbali.

Hivyo naomba usahihishe jamii kwenye makala hizo. Kipala (majadiliano) 12:43, 13 Juni 2022 (UTC)Reply

sawa Mohamed mfuu (majadiliano) 19:52, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
Nimeona umeshanaza, asante!! Ni afadhali kutaja nchi, hivyo unda jamii ya nchi au utumie jamii ya nchi kama ipo tayar (utaziona juu kwenye Jamii:Uwanja wa Ndege). Mfano kwa Uwanja wa ndege wa Saurimo tafadhali uunde "Jamii:Viwanja vya ndege nchini Angola", ndani yake unaweka tu:
[[Jamii:Uwanja wa Ndege|A]] (herufi "|A" - hapa uweke herufi ya kwanza ya nchi ijipange ndani ya orodha sawasawa) na [[Jamii:Usafiri wa Angola]], ndani yake "Jamii:Angola". Yote mengine itajiingiza. Kipala (majadiliano) 21:25, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
sawa nafanya hivyo Mohamed mfuu (majadiliano) 21:29, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
Ila jamii ya viwanja vya ndege angola hakuna Mohamed mfuu (majadiliano) 21:32, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
Mfano kwa Uwanja wa ndege wa Saurimo futa [[Jamii:Uwanja wa Ndege]] badala yake andika [[Jamii:Viwanja vya ndege nchini Angola]]", utasave. Sasa bofya jamii mpya, hariri na ndani yake unaweka tu: [[Jamii:Uwanja wa Ndege|A]] (herufi "|A" - hapa uweke herufi ya kwanza ya nchi ijipange ndani ya orodha sawasawa) na [[Jamii:Usafiri wa Angola]]; kama jamii:Usafiri wa Angola inaonekana nyekundu basi bofya na weka ndani yake "[[Jamii:Angola]]. Yote mengine itajiingiza. Kipala (majadiliano) 21:40, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
Asante sana nimeweza kufanya hivyo Mohamed mfuu (majadiliano) 21:57, 13 Juni 2022 (UTC)Reply


Nimeona Uwanja wa ndege wa Camaxilo, asante!Fuata hatua hizo:

  1. futa [[Jamii:Uwanja wa Ndege]] na futa pia [[Jamii:Usafiri wa Angola]]
  2. [[Jamii:Viwanja vya ndege nchini Angola]] iko, safi! Ni nyekundu, maana haikuunganishwa. kwa hiyo fanya
  3. bofya [[Jamii:Viwanja vya ndege nchini Angola]], ndani yake weka
  4. [[Jamii:Uwanja wa Ndege|A]] na [[Jamii:Usafiri wa Angola]]halafu
  5. save!
  6. Sasa utaona [[Jamii:Usafiri wa Angola]] ni nyekundu, maana haijaunganishwa na jamii ya juu. Kwa hiyo
  7. bofya [[Jamii:Usafiri wa Angola]] (jamii hii itapokea pia vijamii kuhusu reli za Angola, barabara za Angola, mabandari na meli za Angola) Kipala (majadiliano) 22:03, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
  8. halafu ndani yake weka [[Jamii:Angola]]
Naona umeunda viwanja vya ndege vingi nchini Angola. Idadi kubwa ziko katika "Jamii:Uwanja wa ndege" ambako hazitakiwi (maana baadaye jamii yenye majina mengi mno haisaidii kitu). Nashukuru ukipitilia zota, kuondoa "Jamii:Uwanja wa ndege" . Badala yake weka "Jamii:Viwanja vya ndege nchini Angola".Kipala (majadiliano) 23:16, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
sawa kwaiyo makala amabzo nimeweka jamii ya Uwanja wa ndege niondoe Mohamed mfuu (majadiliano) 23:18, 13 Juni 2022 (UTC)Reply
Tazama pia katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Hifadhi_Maalum_ya_Hakiliotsy , inaonekana kuna tafsiri ya kompyuta ama kutokuelewa maana ya maneno kama site ila pia kama ukiona kuna badhi ya maneno hujayaelewa ni bora ya kuyaacha ama kuomba msaada kabla ya kuchapisha makala yako,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 14:17, 14 Juni 2022 (UTC)Reply
saw Mohamed mfuu (majadiliano) 18:39, 14 Juni 2022 (UTC)Reply

Muswada zako hariri

Nakupongeza kwa mtindo wako ya kutangulia kuweka muswada kwanza kabla ya kupeleka makala. Ninavyoona kuna bado dalili za tafsiri ya kompyuta, muundo wa sentensi zisizoeleweka. Labda usome yote tena na ujiulize kama unaelewa kila kitu, hii itasaidia kutambua yale ambayo bado haieleweki. Kipala (majadiliano) 17:56, 8 Aprili 2023 (UTC)Reply

sawa, ahsante Mohamed mfuu (majadiliano) 17:59, 8 Aprili 2023 (UTC)Reply