Amazon (kampuni)
Amazon.com, Inc. (inafanya biashara kama Amazon) ni kampuni ya Marekani yenye makao makuu Seattle, Washington, ambayo ilianzishwa na Jeff Bezos tarehe 5 Julai 1994.
Kampuni hiyo ndiyo kampuni kubwa kabisa duniani ya uuzaji wa bidhaa kwenye intaneti. Kwa kipimo cha mapato na mtaji wa soko, na ni ya pili baada ya Alibaba Group kwa jumla ya mauzo.
Tovuti ya amazon.com ilianza kama duka la vitabu mtandaoni na baadaye ilianza kuuza video, muziki, michezo ya video, nguo, samani, vyakula, vito n.k.
Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya kuchapisha, Amazon Publishing, studio ya filamu na televisheni, Amazon Studios, inatengeneza bidhaa za elektroniki kama vile Kindle, Echo n.k.
Amazon ina maduka ya rejareja katika nchi za Marekani, Uingereza, Ireland, Ufaransa, Canada, Ujerumani, Italia, Hispania, Uholanzi, Australia, Brazili, Japan, China, India, Mexico, Singapore na Uturuki.
Mnamo mwaka 2015, Amazon iliipita kampuni ya Walmart kama kampuni ya uuzaji wa rejareja yenye thamani kubwa zaidi nchini Marekani. Amazon ni kampuni ya pili ya thamani zaidi duniani (nyuma ya Apple tu), kampuni kubwa ya intaneti kwa mapato duniani, na baada ya Walmart, mwajiri wa pili mkubwa nchini Marekani.
Mwaka wa 2017, Amazon ilinunua Whole Foods Market kwa $ bilioni 13.4. Mnamo Septemba 4, 2018, Amazon ilikuwa na thamani ya dola za Marekani trilioni 1.
Kampuni tanzu
haririAmazon inamiliki zaidi ya kampuni tanzu 40, ikiwa ni pamoja na Zappos, Shopbop, Diapers.com, Kiva Systems (sasa inaitwa Amazon Robotics), Audible, Goodreads, Teachstreet na IMDb.[1]
A9.com
haririA9.com ni kampuni inayojihusisha na utafiti na teknolojia tangu mwaka 2003. [2]
Amazon Maritime
haririAmazon Maritime, Inc. ni kampuni inayomiliki meli zinazosafirisha bidhaa za Amazon toka China hadi Marekani.[3]
Amazon Translate
haririAmazon Translate ni kampuni inayotumia teknolojia ya mashine ya kutafsiri.
Audible.com
haririAudible.com ni kampuni inayouza bidhaa za burudani ya masikioni kama vile vitabu, vipindi vya televisheni, n.k. Amazon iliinunua kampuni hii kwa dola za Kimarekani milioni $300.[4]
Beijing Century Joyo Courier Services
haririBrilliance Audio
haririComiXology
haririCreateSpace
haririCreateSpace ni kampuni inayotoa huduma kwa waandishi, wachapishaji, watengeneza filamu na kampuni za muziki. Kampuni hii ilikuwa kampuni tanzu ya Amazon mwaka 2009.[5]
Goodreads
haririLab126
haririShelfari
haririTwitch
haririWhole Foods Market
haririWhole Foods Market ni kampuni inayouza vyakula visivyo na kemikali zenye kuleta madhara kwa binadamu. [6]
Junglee
haririMarejeo
hariri- ↑ "Amazon Jobs – Work for a Subsidiary". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 1, 2014. Iliwekwa mnamo Oktoba 27, 2014.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McCracken, Harry, "Amazon's A9 Search as We Knew It: Dead!", PC World. September 29, 2006. Retrieved September 6, 2012.
- ↑ Steele, B., Amazon is now managing its own ocean freight, engadget.com, January 27, 2017, accessed January 29, 2017
- ↑ Sayer, Peter. "Amazon buys Audible for US$300 million", PC World, January 31, 2008.
- ↑ "Independent Publishing with CreateSpace". CreateSpace: An Amazon Company. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Novemba 26, 2013. Iliwekwa mnamo Januari 22, 2017.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Quality Standards". Whole Foods Market.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi
- Kampuni za Amazon
- Jinsi ya kufikisha malalamishi kwa Amazon tarishi anopokosa kulifikisha furushi lako Archived 27 Juni 2019 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amazon (kampuni) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |