Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

TangazoEdit

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 19:46, 5 Aprili 2020 (UTC)

Mwaliko wa kutoa maoni yako kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na NidhamuEdit

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa na kuunga mkono wazo hilo. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuoanisha vitu vya msingi vya kimwongozo vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano katika Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kujaribu kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) au utumiaji wa Wikipedia, na pia pale wanawikipedia wanapowasiliana ndani ya tovuti ya Wikipedia yenyewe au wanapokutana ana kwa ana katika warsha na mikutano mbalimbali ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kutokea kwa baadhi ya matukio kwa baadhi ya Wanawikimedia anbapo katika tafiti iliyofanywa mwaka 2015 , ilionekana baadhi ya Wanawikimedia walikuwa wakikumbana na unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huona unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 29th April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Tanzania (Dar es Salaam) ili tuweze kujadiliana na kubadilishana mawazo, uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia na miradi mingine yake ya Wikimedia Foundation. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuhusu miradi waliyoifanya tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi Mtavangu19:09, 18 Aprili 2020 (UTC)

Makala ya Muungano, herufi kubwaEdit

Asante kwa mchango wako. Tafadhali usitumia tene HERUFI KUBWA, hazipendezi na hazitakiwi katika fomati yetu (isipokuwa vifupisho kama TUKI, NATO, UM). Asante. Kipala (majadiliano) 07:36, 30 Mei 2020 (UTC)

Masahihisho ya ukurasa wa mtumiajiEdit

Tafadhali weka vyanzo kwenye kipengere cha tuzo kwenye makala yako.

Jamii na interwikiEdit

Asante kwa michango, lakini umesahau interwiki (Msaada:Interwiki) na jamii ulizotumia hazisaidii. Ukiandika chini ya makala Jamii:Wanawake wa Aisilandi (katika mabano mraba yaani [[Jamii:Wanawake wa Aisilandi]]) afadhali; vizuri zaidi ingekuwa [[Jamii:Wanamuziki wanawake wa Aisilandi]]. Baada ya kuhifadhi makala ungeona jamii hizo kwa rangi nyekundu maana hazikuunganishwa bado katika mfumo wa jamii. Hapa uatendelea katika hatua ya pili ambayo ni kuunganisha na jamii mbili za juu: fungua jamii uliyounda, mfano Jamii:Wanawake wa Aisilandi na ndani yake unaandika [[Jamii:Watu wa Iceland]] (maana inaonekana tumetumia tahajia zote mbili) halafu pia [[Jamii:Wanawake wa Ulaya]].

Kama umetumia [[Jamii:Wanamuziki wanawake wa Aisilandi]] utahitaji kuunganisha na:

  • [[Jamii:Wanamuziki wa Aisilandi]], inayohitaji kuunganishwa tena na [[Jamii:Watu wa Iceland]] na pia
  • [[Jamii:Wanamuziki nchi kwa nchi]]

Baada ya hatua hizo umekamilisha makala. Kipala (majadiliano) 12:01, 29 Machi 2021 (UTC)

Naona bado hatujaelewana. Ni vizuri kwamba umempanga Jamii:Wanamuziki wanawake wa Aisilandi. Hii ya "Watu wa Iceland" inawezekana, ingawa kwa nchi yenye makala mengi ya watu haisaidii sana maana utapata mwishono orodha ndefu sana ya majina; ingetosha kuweka Jamii:Watu wa Iceland ndani ya Jamii:Wanamuziki wanawake wa Aisilandi. Ingawa ningependelea upange Jamii:Wanamuziki wanawake wa Aisilandi katika jamii mpya "Wanamuziki ya Aisilandi" na hiyo ndani ya zote mbili "Watu wa Iceland" na pia "Wanamuziki nchi kwa nchi". Kama hujaelewa, tafadhali uniulize.
Pia naona hujaunganisha bado na interwiki. Nimekupa pale juu ukurasa wa msaada:Interwiki, tafadhali ufuate hatua zinazotajwa. Kipala (majadiliano) 12:51, 29 Machi 2021 (UTC)
Ndugu, naona unajitahidi kuandika vizuri. Ila suala la jamii linakusumbua bado. Ukianzisha jamii ya wanamuziki wanawake, hiyo ni ndani ya jamii za wanamuziki na za wanawake, si kinyume! Yaani wewe unaweka jamii ya wanamuziki (wa jinsia zote) ndani ya ile ya wanamuziki wanawake... Kwa mfano, Wagogo ni Watanzania, lakini si Watanzania wote ni Wagogo! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:43, 31 Machi 2021 (UTC)

HongeraEdit

Napenda kukupongeza kwa juhudi zako katika Wikipedia. Endelea kuangalia kama pengine ninarekebisha michango yako ili uzidi kukomaa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:29, 16 Aprili 2021 (UTC)

Asante, nakupongeza pia kwa ujuzi ulionao. Nafuatilia marekebisho yako na ubarikiwe kwa kazi unayoifanya. Amani iwe kwako pia! -- Rwebogora (majadiliano) 14:50, 16 Aprili 2021 (UTC)

Miji ya UgandaEdit

Nazidi kukupongeza. Tafadhali, chini ya makala za aina hii, bandika kama ifuatavyo: ==Marejeo== {{reflist}} {{mbegu-jio-Uganda}} [[Jamii:Miji ya Uganda]] [[Jamii:Wilaya ya Amuru]] [[Jamii:Africa Wiki Challenge 2021 in Tanzania]] Asante sana kwa ushirikiano. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:50, 23 Julai 2021 (UTC)

Bila shaka, baadaye badilisha jina la wilaya! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:51, 23 Julai 2021 (UTC)

Karibu tenaEdit

Tuliku"miss" sana. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:54, 24 Novemba 2021 (UTC)

Asante sana! Rwebogora (majadiliano) 20:49, 24 Novemba 2021 (UTC)