NATO (kifupi cha North Atlantic Treaty Organisation; kwa Kifaransa: OTAN, Organisation du Traité de l'Atlantique Nord, yaani Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini) ni ushirikiano wa kujihami ya kambi ya magharibi. Inaunganisha nchi 28 za Ulaya pamoja na Marekani na Kanada. Nchi wanachama zimeahidi kuteteana kama moja inashambuliwa na nchi ya nje. Makao makuu yapo Brussels.

Nchi wanachama wa NATO mwaka 2020 kwa rangi ya buluu.
Uenezi wa NATO hadi mwaka 2020.

HistoriaEdit

NATO ilianzishwa mwaka 1949 wakati wa vita baridi kama maungano ya nchi za Ulaya ya magharibi pamoja na Marekani dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na nchi shiriki zake katika Mapatano ya Warshawa. Nchi wanachama wa kwanza walikuwa Marekani, Ubelgiji, Uholanzi, Luxemburg, Ufaransa, Uingereza, Kanada, Ureno, Italia, Norwei, Denmark na Iceland. 1952 Ugiriki na Uturuki zilijiunga pia zikafuatwa na Ujerumani ya Magharibi.

Baada ya mwisho wa vita baridi nchi zilizokuwa chini ya Umoja wa Kisoveti kama sehemu ya kambi ya kikomunisti zilijiunga na NATO kuanzia mwaka 1999. Ndizo Hungaria, Ucheki, Poland (1999), halafu Estonia, Latvia, Lithuania, Slovenia, Slovakia, Bulgaria, Romania (2004), Kroatia, Albania (2009), Montenegro (2017), Masedonia Kaskazini (2020).

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu: