Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:58, 28 Juni 2021 (UTC)Reply

Please, this is not the English edition! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:58, 28 Juni 2021 (UTC)Reply
Please, this is not the Kiswenglish edition! Peace to you! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:33, 22 Aprili 2022 (UTC)Reply

Vyanzo vya Kiingereza

hariri

Salamu, napenda kukukumbusha kwamba vyanzo vinavyotokana na link za Wikipedia ya Kiingereza haviruhusiwi kutumika kama marejeo katika Wikipedia ya Kiswahili, Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 08:45, 25 Mei 2022 (UTC)Reply

Sawa, kwahiyo kama vyanzo havipo kwenye kiswahili tusiweke? Super8 Devs (majadiliano) 08:52, 25 Mei 2022 (UTC)Reply
Naona Idd Ninga hajakujibu, hivyo wewe umeendelea kuweka vyanzo vinavyotokana na link za Wikipedia ya Kiingereza ambavyo haviruhusiwi. Hilo ni kosa. Unatakiwa kuchukua vyanzo vilivyotumiwa na Wiki ya Kiingereza na kuvitumia kama vyetu, si kuweka kiungo cha kwenda kuvitafuta katika Kiingereza. Sijui kama nimeeleweka. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:57, 25 Mei 2022 (UTC)Reply

Kuteua mada na kuazisha makala

hariri

Ndugu, naona umeandaa makala kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Je umeshatambua kwamba mada kadhaa zina makala tayari? Naona sasa tu kwamba wingu na makaa ya mawe ziko tayari, labda nyingine. Ukitafuta mada labda uangalie hapa: makala za msingi za kamusi elezo na pia kwenye makala kuhusu Tanzania zilizopo kwa Kiingereza lakini haziko bado swwiki, mfano hapa: Majadiliano ya mtumiaji:Kipala/List Category Tanzanian people en. Kipala (majadiliano) 21:23, 7 Aprili 2023 (UTC)Reply

Sawa kiongozi ngoja nirekebishe, Ahsante Super8 Devs (majadiliano) 07:32, 8 Aprili 2023 (UTC)Reply
Unaweza kuunganisha Mkala hii hapa ya Usanisinuru bandia na Wikipedia ya Kiingereza, ili isaidie wahariri wengine kuona ni kitu gani ulikusudia kuandika na wengine wakafanya maboresho,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 12:36, 13 Aprili 2023 (UTC)Reply
Sawa, naishughulikia hivi karibuni. Ahsante Super8 Devs (majadiliano) 08:36, 15 Aprili 2023 (UTC)Reply

Kuzuiwa

hariri

Ndugu, nimekuzuia kwa sababu umeandika makala nyingi harakaharaka mno. Ukitaka kuendelea, kwanza ahidi kurekebisha makala zako zieleweke. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:03, 21 Aprili 2023 (UTC)Reply

Ndio, Naahidi kurekebisha makala zangu, Ahsante. Super8 Devs (majadiliano) 07:11, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply
Inabidi sasa kufuta makala zako nyingi kwa sababu bado zipo vibaya,acha kwanza makala katika ukurasa wako wa mtumiaji, na kabla ya kuzichapisha kwenda makala kuu,omba kwanza msaada wa mtu azipitie ili kuona kama zina ubora, hiyo itapunguza mrundikano wa makala zisizo na ubora,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 07:21, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply
Nitafanya hivyo, Ahsante. Super8 Devs (majadiliano) 07:30, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply
Pia angalia aina ya kigezo cha mbegu unachoweka kama kinaendana na Makala husika, mfano makala zako nyingi, umeweka kigezo cha JIO wakati ilitakiwa kuweka kigezo cha MTU,Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 07:38, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply
Sawa. Super8 Devs (majadiliano) 07:57, 22 Aprili 2023 (UTC)Reply