Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Asante kwa michango yako, mifupi lakini sahihi. Ili kuiboresha, angalia nilivyoisahihisha karibu yote namna moja. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:10, 19 Oktoba 2019 (UTC)Reply
Karibu, umeanza kwa mbio. Tafadhali usisahau kupanga kila makala katika jamii zake (category). Kipala (majadiliano) 23:10, 5 Novemba 2019 (UTC)Reply
Pia pembeni uuanganishe nakala ya Kiswahili na zile za lugha nyingine. Amani kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:51, 6 Novemba 2019 (UTC)Reply
Pia zingatia kuweka marejeo. Hongera kwa mwanzo mzuri. Amani Czeus25 Masele (majadiliano) 18:13, 2 Aprili 2020 (UTC)Reply

Ukurasa wa Mtumiaji hariri

Habari karibu, ni jambo jema kuandika walau chochote katika ukurasa wako, angalia kiungo hapa chini ili kuendelea
https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mtumiaji:UmojaWetu&action=edit&redlink=1

Czeus25 Masele (majadiliano) 18:16, 2 Aprili 2020 (UTC)Reply

Bienvenue! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:31, 3 Aprili 2020 (UTC)Reply

Tangazo hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo


Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia


Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 17:06, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Istilahi za kompyuta hariri

Ndugu umechangia mengi kwa kuongeza istilahi za kompyuta. Asante! Naona tatizo kidogo ukiendelea kutumia pekee ile orodha ya Microsoft miaka ya 2000. Ambayo ni tatizo maana wakati ule Microsoft na Ubuntu / Open Movement walianzisha istilahi bila kuwasiliana kati yao, tena hawakusambaza na wengine waliounda mengine. je unajua jinsi gani kutafuta majina mbadala na kuunda makala za kuelekeza? Tena kuna kamusi kubwa ya kompyuta ya TUKI (ambayo kwa bahati mbaya ilikuwa kazi ya bure maana ilitungwa Kiswahili - kiingereza na wote wanatafuta kinyume; ninajaribu kupata data zake).

HALAFU ni vema ikiangalia pia jinsi gani watu wanavyojadili michango yako. Injua jinsi ya kufuatiliua? Mfano makala yako "Ubaridi Hewa" ilijadiliwa na kubadilishwa maana istilahi haieleweki vizuri. Sasa umeleta pia "Ubaridi maji" ambayo ni tatizo lilelile (ubaridi ni coldness, si cooling). Nashukuru tukiweza kuwasiliana. Kipala (majadiliano) 17:25, 20 Oktoba 2020 (UTC)Reply

Hujambo. Je, unaweza kunituma Kamusi kubwa ya kompyuta ya TUKI kwa PDF tafadhali ? Kijisanduku changu ni tobin.poubelle@gmail.com . Asante sana kwa marekebisho yako. Samahani, Kiswahili si lugha ya mama yangu. Lakini nitajaribu kuboresha kiswahili changu. UmojaWetu (majadiliano) 21:41, 21 Oktoba 2020 (UTC)Reply

Subiri kidogo. Najitahidi kupata faili yake. Labda pia hoja zuri (baadaye) ni kukazia makala za meta:List_of_articles_every_Wikipedia_should_have/Expanded#Information_technology,_89 Kipala (majadiliano) 20:20, 21 Oktoba 2020 (UTC)Reply
Habari, naomba ama uwezeshe "email this user" hapa kwenye ukurasa wako, au niandikie baruapepe. 22:56, 24 Oktoba 2020 (UTC)
Niliwezesha barua pepe toka kwa watumiaji wengine katika mapendekezo sasa. 23:00, 25 Oktoba 2020 (UTC)