Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo - hata kuitafsiri kutoka katika Wikipedia kwa lugha nyingine. Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wa sanduku la mchanga. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike pekee kwenye ukurasa wako wa mtumiaji baada ya kufungua akaunti. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho. Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje
  • wala matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, MediaWiki Content Translation, etc.)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Idd ninga (majadiliano) 09:02, 19 Juni 2021 (UTC)

Uhariri wa makalaEdit

Habari ndugu @Zabron'sPedia,

Pongezi kwa kazi nzuri na kubwa unayoifanya. Tafadhari zingatia kutokutumia tafsiri za kompyuta katika makala, hakiki makala yake kuwa inaeleweka kabla ya kuichapisha.

Pia namna ya uwekaji viungo vya marejeo naona una shida kama unachangamoto tafadhari tuwasiliane kwa msaada. Asante. MagoTech Tanzania (majadiliano) 16:53, 21 Juni 2021 (UTC)

Umakini na lugha sahihiEdit

Mpendwa, umeleta makala ambazo zina Kiswahili kibaya tena tafsiri bila kutafakari. Mfano Alexander Michaeletos hakika si tena mwigizaji mtoto, maana sasa anakaribia umri wa miaka 20. Kwa hiyo usitafsiri bila kutumia akiloi ya wastani. Kama makala ya kiingereza ina kasoro dhahiri, usitafsiri mambo yasiyo na maana, angalau sahihisha maudhui ili ipate maana. Katika Graham Payn ulitumia lugha isiyo na maana kabisa, sijui kama udhaifu wako uko upande wa kiingereza au Kiswahili au pande zote mbili?? Sentensi kama "Katika umri wa miaka 14, alijaribu Noël Coward na Charles B. Cochran kurekebisha Maneno na Muziki (1932)" ni nini? Nahisi unatumia google translate na kumaga matokeo bila kuisoma tena. Ninakuonya sasa, ukirudia nitakuzuia katika wikipedia hii. Sasa tafadhali rudi kwenye makala ulizooleta na kuzisoma halafu kuzirekebisha. Kipala (majadiliano) 19:48, 24 Juni 2021 (UTC)

Ndugu, pamoja na hayo, Kipala ametukumbusha kwamba hatutakiwi kuweka kama tanbihi makala ya Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine, bali vyanzo vyenyewe vya nje. Nakutakia utekelezaji mwema na amani ya Bwana. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:57, 29 Juni 2021 (UTC)
Asante kwa kujirekebisha. Sasa endelea na kuboresha makala zako. Afadhali chache lakini nzuri. Kwa mfano, unapoandika chini ==Marejeo== usisahau kuweka {{reflist}} ili tanbihi zitokee mahali pake. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:45, 30 Juni 2021 (UTC)

VyanzoEdit

Salamu ndugu, tazama tena katika makala hii https://sw.wikipedia.org/wiki/Mauaji_ya_halaiki_ya_Isaaq kuna onekana kuwepo kwa vyanzo ambavyo vinatokana na link za makala ya Wikipedia ya Kiingereza, vyanzo hivi havitakiwi , ni vyema kuiboresha makala katika upande huo,Amani Sana Idd ninga (majadiliano)

KukuzuiaEdit

Nimeondoa zuio. Kuhusu makala zako ambazo uzipitie upya, angalia zile zilizowekewa lebo "tafsiri kompyuta". Asante kwa moyo wako. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:38, 18 Agosti 2021 (UTC)

Ndugu, mbona umeanza tena bila kutimiza ahadi yako ya kupitia upya makala zako zisizoeleweka? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:09, 18 Agosti 2021 (UTC)
Angalia vizuri, kwa mfano: Mihuri ya mapato ya Zanzibar. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:09, 18 Agosti 2021 (UTC)

Salamu ndugu Zabron'sPedia , ni vyema sana kama utakuwa unaunganisha makala yako ya kiswahili na lugha ya kiingereza ili iwe rahisi kwa wahariri wengine kuifikia na kuifanyia marekebisho, amani sana Idd ninga (majadiliano)

Pitia Makala ZakoEdit

Angalia mfano wa makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Chama_cha_Usawa_Binafsi_cha_Tanzania haijaungnishwa na lugha nyingine, inakuwa ngumu sana kufahamu ni kitu umeandika na pia ni ngumu kuipata ili kuifanyia marekebisho, pia kabla ya kuendelea na makala nyingine hebu hakikisha kwanza unapitia makala ambazo ulitakiwa kurekebisha ,uwepo wa makala zenye matatizo utasababisha sasa ufungiwe tena na hata kama ukifunguliwa itakubidi kurekebisha makala zilizopoita pamoja na kufuata maelekezo unayopewa kabla ya kuendelea na makala nyingine, kama unachngamoto katika uundaji wa makala jaribu kuuliza, sote badi tunajifunza kutumia Wikipedia,Amani sana Idd ninga (majadiliano)

Kuondoa VyanzoEdit

Katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Benki_ya_KCB_Tanzania vyanzo vipo katika makala ya KLiingereza ila ya Kiswahili umeviondoa, inaoneka una copy kwa mtindo tofauti na ule unaotakiwa,fuata taratibu zote za kutoa makala katika lugha ya Kiingereza na kuja kuitafsiri katika lugha ya Kiswahili, Idd ninga (majadiliano)

Taarifa ya zuioEdit

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Ndugu umeonywa mara kadhaa. katika UKIMWI nchini Uganda‎ umemwaga tena matini kutoka google translate bila kujali na kwa masahihisho machache mno. Tokeo ni aibu. Kipala (majadiliano) 07:56, 25 Agosti 2021 (UTC)