Mansueti wa Urusi (alifariki 435 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji wa Urusi (leo nchini Tunisia).

Alifariki pamoja na askofu Papiniani wa Vita kwa kuchomwa mwili mzima kwa vyuma vya moto katika dhuluma ya Genseriki, mfalme wa Wavandali[1].

Habari zake zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Novemba[2][3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.