Mapatano ya Laterano

Mapatano ya Laterano kati ya Ufalme wa Italia na Ukulu mtakatifu yanaitwa hivyo kwa sababu yalisainiwa katika jumba la Laterano tarehe 11 Februari 1929.

Ramani ya Mji wa Vatikani.

Lengo lake lilikuwa kumaliza suala la Roma lililovuruga Italia tangu mwaka 1870, nchi hiyo ilipoteka mji huo uliotawaliwa na Mapapa kwa karne nyingi.

Kwa mapatano hayo, Papa alikubali mji ubaki mikononi mwa Ufalme, isipokuwa mtaa wa Vatikano na majengo mengine machache. Ndivyo ilivyoundwa na kukubalika kimataifa nchi huru ya Mji wa Vatikani iliyomwezesha Papa kuwa huru katika kuongoza Kanisa Katoliki duniani kote.

Mapatano hayo yaliheshimika hata baada ya serikali ya Ufashisti kuanguka, Italia kugeuka Jamhuri na katiba mpya kutungwa. Tena hiyo ilijumlisha mapatano hayo ndani yake[1].

Tanbihi hariri

  1. The Constitution of the Italian Republic, article 7. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-12. Iliwekwa mnamo 2016-05-04.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mapatano ya Laterano kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.