Open main menu

Katika imani ya KikatolikiEdit

Kwa msingi huo, ukulu unamwakilisha Papa kama kiongozi wa Kanisa Katoliki lote duniani na kuhusiana na dogma ya kwamba ana karama ya kutodanganyika anapofundisha "rasmi" (kwa Kilatini "ex cathedra", yaani "kutoka ukulu") kama mkuu wa kundi la maaskofu.

Katika liturujiaEdit

Sikukuu ya ukulu huo inaadhimisha kila mwaka tarehe 22 Februari kwa jina la Ukulu wa Mtume Petro, anayeaminiwa kuwa ndiye aliyewarithisha Mapapa mamlaka yake kama mkuu wa Mitume wa Yesu.

Katika sheria za KanisaEdit

Kadiri ya Mkusanyo wa Sheria za Kanisa la Kilatini (kanuni 361), "Ukulu mtakatifu" ni jina rasmi linalotumika kuwamaanisha Papa na miundo yote inayomsaidia kuongoza Kanisa Katoliki duniani ikiwa na makao makuu mjini Roma.

Ukulu usipokuwa na PapaEdit

Wakati Kanisa linapobaki halina Papa (kutokana na kifo au kujiuzulu), uongozi wake unashikwa na Kundi la Makardinali ambalo pia lina wajibu na haki ya kumchagua mwandamizi wake.

Katika mafungamano ya kimataifaEdit

 
Nchi zenye uhusiano na Ukulu mtakatifu.      Uhusiano wa kibalozi      Uhusiano mwingine      Bila uhusiano rasmi

Ukulu mtakatifu una hadhi ya nafsi ya kisheria katika sheria za kimataifa kutokana na umbile lake, mapokeo ya historia na mahitaji ya utume wake.

Ukulu mtakatifu unawakilisha kwa pamoja Kanisa Katoliki na nchi huru ya Mji wa Vatikani (ambayo iko chini ya mamlaka yake) katika mafungamano ya kimataifa na nchi yoyote duniani na miundo ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, ambapo unatambulika kama mojawapo kati ya watazamaji wa kudumu.

Ukulu mtakatifu na VatikaniEdit

Kisheria, Ukulu mtakatifu ni tofauti na Mji wa Vatikani ambayo ni nchi huru inayotawaliwa na Papa.

Eneo dogo la nchi hiyo (kilometa mraba 0.44) linadaiwa na kutosha ili kuhakikisha uhuru wa miundo ya Kanisa katika kutekeleza majukumu yake.

Mabalozi wanaowakilisha nchi huru nyingine (180, mwanzoni mwa mwaka 2013) wanatumwa kwa Ukulu mtakatifu, si kwa nchi ya Vatikani.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit