Mapendo ya kiuchumba

Mapendo ya kiuchumba ni aina mojawapo ya mapendo kati ya binadamu.

Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu mapendo

Moyo katika mapokeo ya Ulaya
ni mchoro unaowakilisha mapendo.
Vipengele Msingi
Mapendo kadiri ya sayansi
Mapendo kadiri ya utamaduni
Upendo (fadhila)
Upendo safi
Kihistoria
Mapendo ya kiuchumba
Mapendo ya kidini
Aina za hisia
Mapendo ya kiashiki
Mapendo ya kitaamuli
Mapendo ya kifamilia
Mapendo ya kimahaba
Tazama pia
Mafungamano ya binadamu
Jinsia
Tendo la ndoa
Maradhi ya zinaa
Siku ya wapendanao

Katika maana yake halisi, aina hiyo ni ya maandalizi kwa ajili ya ndoa.

Hapo zamani mara nyingine hakuwepo na mapenzi kwanza, kwani mvulana na msichana walifikia kuoana bila kuwepo kwanza uchumba.

Lakini kwa sasa, kutokana na maendeleo na akili kupanuka zaidi, kwa kawaida hakuna anayeoa au anayekubali kuolewa bila kumfahamu mchumba wake kwanza.

Ule muda wa kuzoeana, ndio wa mapendo ya kiuchumba, kwani haitoshi, k.mf. kumtamkia tu mpenzi wako kwamba ungependa awe mama watoto wako bila ya kuzijua silika, tabia, hisia zake na kadhalika. Ni vilevile upande wa pili.

Muda wa kuchumbiana ndio muda ambao wote wawili wanatakiwa kuwa makini sana, kila mmoja amsome mwenzie na kujirekebisha ili kuwezesha ndoa kudumu hata itakapojaribiwa na maisha.

Bahati mbaya, mara nyingi vijana hawapati malezi au msaada wowote wa kufaa upande huo. Sehemu nyingi wanaelekezwa tu namna ya kupunguza hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa au kupata mimba isiyotarajiwa, kama kwamba ngono inawafaa katika hatua hiyo au haiepukiki kabisa.