Maretadu
Maretadu ni kata ya Wilaya ya Mbulu Vijijini katika Mkoa wa Manyara, Tanzania.
Kata ya Maretadu | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Manyara |
Wilaya | Mbulu |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 15,200 |
Hali ya hewa huko ni nzuri yenye misimu ya mvua na ya kiangazi kwa muda unaoeleweka. Masika huanza mwezi Novemba hadi Mei. Baada ya hapo ni kiangazi na vuli za kawaida.
Kata hiyo ina vijiji kama Endamasak, Maretadu Juu, Maheri, Qamtananat, Maretadu Chini na Garkawe.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 15,200 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,343 waishio humo.[2]
Wakazi hasa ni wa makabila ya Wairaqw na Watatoga.
Shughuli kubwa ya kiuchumi ya wakazi wa hapo ni kilimo na ufugaji. Kilimo kinachoendeshwa sana ni cha mahindi, maharage, ngano, dengu, alizeti, mtama, n.k. Ufugaji ni wa ngombe, mbuzi, kondoo, punda na kuku.
Kata ya Maretadu ina shule kadhaa za msingi kama Maretadu juu, Maretadu Chini, Hayedarer, Simha, Qamtananat. Shule ya Msingi Maretadu Juu ni ya miaka mingi na imeanza mwaka 1953. Tokea hapo imeendelea kutoa wasomi wengi na inafanya vizuri hadi sasa.
Pia kuna Shule za Sekondari kama Shule ya Sekondari Maretadu, shule ya Sekondari Maretadu Juu, na Shule ya Sekondari Jakaya Kiwete.
Wasomi kadhaa wametoka katika kata hiyo. Baadhi ni Prof. Joshua Doriye aliyepata kushika nyadhifa mbalimbali serikalini hadi ngazi ya Katibu Mkuu wa Wizara, Tume ya Mipango na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam. Pia yuko Dr. Bertha Maegga, wa Taasisi ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI).
Maretadu hata hivyo inahitaji maendeleo katika nyanja mbalimbali ili ipate kusonga mbele kutoka hapo ilipofikia.
Marejeo
haririKata za Wilaya ya Mbulu Vijijini - Mkoa wa Manyara - Tanzania | ||
---|---|---|
Bashay | Dinamu | Dongobesh | Endahagichan | Endamilay | Eshkesh | Geterer | Gidhim | Haydarer | Haydom | Labay | Maghang | Maretadu | Masieda | Masqaroda | Tumati | Yaeda Ampa | Yaeda Chini |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maretadu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|