Maria Alfonsa Matathupadathu

Maria Alphonsa Muttathupadathu (Kudamalloor, karibu na Kottayam, huko Kerala[1]19 Agosti 1910 - Bharananganam, 28 Julai 1946) alikuwa bikira Mfransisko wa Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar nchini India.

Kaburi la Mt. Alfonsa.

Ili asiolewe kwa shuruti, alijichoma mguu kwa kuuweka motoni. Kisha kupokewa katika shirika ya Waklara wa Kimalabari, alimtolea Mungu maisha yake yote akiwa mgonjwa karibu mfululizo.

Alitangazwa mwenye heri na Papa Yohane Paulo II tarehe 8 Februari 1986 akatangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 12 Oktoba 2008.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. ""St. Alphonsa – Our Patroness" St. Alphonsa Church, Bangalore". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-02-22. Iliwekwa mnamo 2015-02-06.
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.