Maria Ana wa Yesu (jina kamili la Kihispania ni Mariana de Jesús Paredes y Flores; Quito, Ekwador, 31 Oktoba 1618 - Quito, 26 Mei 1645, alikuwa bikira wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko aliyejitoa kwa Kristo na kuhudumia Waindio na watu kutoka Afrika fukara.

Mchoro wa Francisco Sylverio de Sotomayor (karne ya 18) kuhusu Mariana de Jesús, Azucena de Quito, Heroina Nacional y Virgen Penitente.

Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 20 Novemba 1853. Papa Pius XII akamtangaza mtakatifu tarehe 4 Juni 1950, akiwa mtu wa kwanza kutoka Ekwador, na Mfransisko wa kwanza kutoka Amerika Kusini kutangazwa mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 26 Mei[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.