Martiniani, Saturiani na wenzao

Martiniani, Saturiani na wenzao wawili walikuwa wote ndugu; ni kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.

Wote waliongokea Ukristo kwa njia ya Masima bikira, mtumwa mwenzao nyumbani mwa Mvandali fulani.

Baada ya kutoroka, walijiunga na monasteri huko Thabraca, lakini walikamatwa na, baada ya kupigwa kwa fimbo nene hadi kutokeza mifupa kwa sababu ya kuwa imara katika imani sahihi, walipelekwa uhamishoni Caprapicta, kati ya Wamori, walipohukumiwa kufa kwa kuwa walivuta wengine katika Ukristo [1], wakauawa pamoja na wenzao pengine 361, wakiwemo Saturnini, Nerei na Serea [2][3].

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Oktoba[4][5][6][7].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.