Mary Sixtus Busungu (anafahamika kwa jina lake la kisanii kama Mary Msukuma; amezaliwa 5 Februari 1982) ni msanii wa maigizo ya vichekesho na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania. Ni dada wa damu wa mwanamuziki Benjamin wa Mambo Jambo ambaye ameonekana kushiriki naye katika mifululizo ya vichekesho mtandaoni.

Maisha hariri

Mary ni mtoto wa saba kati ya watoto kumi wa marehemu Sixtus Michael Busungu.

Alisoma elimu ya msingi katika shule tofautitofauti kutokana na kuhamishwa kwa wazazi kikazi. Shule alizosoma ni pamoja na Shule ya Msingi Kikombo iliyopo Mpwapwa Mkoani Dodoma, Kibakwe iliyopo mkoani Dodoma, Isenga iliyopo Mwanza Pasiansi, Changanyikeni iliyopo jijini Dar es Salaam na kumalizia Kawawa iliyopo wilaya ya Kinondoni kuanzia mwaka 1990 -1996.

Miaka 1997—2000 alijiunga na elimu ya sekondari ambapo pia alisoma katika shule tofautitofauti. Alisoma Oysterbay Under Maria Management, Tegeta High School zote zipo wilaya ya Kinondoni. Elimu hiyo ya sekondari alikuja kumalizia Mpwapwa sekondari mkoa wa Dodoma.

Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, alishiriki mashindano ya ulimbwende na kushinda Miss Dodoma nafasi ya pili—2003. Baadaye alishiriki Miss Kanda ya Kati na kuibuka mshindi wa nne mwaka huohuo wa 2003, baada ya hapo aliendelea na urembo na kushiriki Miss Morocco—Kinondoni—jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuwa kwenye kumi bora—2005.

Mwaka wa 2005, alisoma kozi ya ukarani katika Chuo cha Splended (Ilala). Baadaye pia aliweza kushiriki katika shindano la Miss Kisura na kuibuka mshindi wa kisura photogenic wa Tanzania 2009. Alianza kazi za ujasiliamali na ubunifu wa mitindo na kushiriki pia kwenye maonyesho ya mitindo ya watu maarufu kama Ally Lemtura, Fatuma Amour na Merinyo wa Africa Sana.

Uigizaji hariri

Viungo vya nje hariri