Masimo wa Chinon
Masimo wa Chinon (pia Maxe, Mexme, Mesme; alifariki Chinon, karibu na Tours, Gaul, leo Ufaransa 470 hivi) alikuwa mmonaki, mfuasi wa Martino wa Tours.
Alijitahidi kukwepa umaarufu, lakini kila alipokwenda watu walikuwa wakimtambua kama mtu wa Mungu[1].
Hatimaye alianzisha monasteri kwenye mto Vienne, alipofariki akiwa mzee sana.
Maisha yake yaliandikwa na Gregori wa Tours katika sura moja ya kitabu De Gloria Confessorum.
Tangu kale hadi leo anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu abati.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |