Mbingu (Kilombero)

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Mbingu

Mbingu ni kata ya Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67512.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 22,717 [1] walioishi humo.

Kuna vijiji vya Vigaeni, Chiwachiwa na Mbingu.

Wakazi wengi ni wakulima wanaolima mahindi, mpunga, ndizi, muhogo, kokoa na mengineyo.

Pia wanajihusisha na uvuvi wa samaki kwenye mito midogomidogo na mabwawa.

Makampun yasiyo ya kiserikal yanayojihusisha na shughul za kilimo yanayopatikana Mbingu ni pamoja na KOKOAKAMIL, OLAM and JATU.

MarejeoEdit

  1. Sensa ya 2012, Morogoro - Kilombero DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-03.
  Kata za Wilaya ya Kilombero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Ching'anda | Chisano | Chita | Idete | Ifakara | Igima | Kalengakelo | Kamwene | Katindiuka | Kibaoni | Kiberege | Kidatu | Kisawasawa | Lipangalala | Lumemo | Mang’ula 'B' | Mang'ula | Masagati | Mbasa | Mbingu | Mchombe | Michenga | Mkula | Mlabani | Mlimba | Mngeta | Mofu | Msolwa Station | Mwaya | Namwawala | Sanje | Signal | Utengule (Kilombero) | Viwanja Sitini


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mbingu (Kilombero) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.