Mlimba ni kata ya Wilaya ya Mlimba katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 23,984 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 38,108 [2] walioishi humo.

Mlimba ni jina la mtu ambaye alikuwa anakaa karibu na chanzo cha mto ambao TAZARA walifanya water intake mbele ya ilipokuwa ofisi ya usafirishaji ya TZR wakati wa ujenzi wa reli. Mzee huyo ndiye aliyesababisha mji kuitwa Mlimba na ule mto kuitwa Mlimba. Alikuwa mzee maarufu na aliwasaidia mafundi waliokuwa wakijenga reli kupata nyama ya porini na samaki ambao walipafanya Mlimba kupendwa sana na wajenzi wale.

Ili kufikia Mlimba kuna aina mbili za usafiri ambazo ni usafiri wa barabara na wa garimoshi ambayo hujulikana kama usafiri wa TAZARA.

Barabara inatokea Dar es Salaam kupitia Morogoro mjini, Mikumi, Ifakara na hatimaye Mlimba. Hiki kipande cha kutoka Ifakara kwenda Mlimba ni barabara ya vumbi.

Tazara ni usafiri wa garimoshi ambao huanzia safari zake Dar es Salaam, Tanzania, na kuishia Kapiri Mposhi, Zambia. Huu ndio usafiri unaotumiwa na asilimia kubwa ya wananchi wanaoishi Mlimba na ni usafiri unaotumika vipindi vyote vya mwaka ikiwemo masika na kiangazi.

Mlimba shughuli kubwa inayotumika kuendesha maisha ya kila siku ni kilimo. Wakazi wa Mlimba wanalima mazao kama mpunga, ufuta, mahindi, viazi, mihogo na kufuga nyuki. Lakini zao lao kuu la chakula na biashara ni zao la mpunga, wakazi wa Mlimba karibia asilimia mia wanalima mpunga na hii ni kutokana na jiografia ya eneo la Mlimba kuwa la bonde kubwa.

Fursa nyingine zinazopatikanika Mlimba ni biashara ya mchele, kilimo cha miti aina ya mitiki na shughuli za uvuvi.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Morogoro - Kilombero DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-03. 
  Kata za Wilaya ya Mlimba - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Ching'anda | Chisano | Chita | Idete | Igima | Kalengakelu | Kamwene | Masagati | Mbingu | Mchombe | Mlimba | Mngeta | Mofu | Namwawala | Uchindile | Utengule


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlimba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.