Meli za mizigo ni meli ambazo hutumika kubeba mizigo mbalimbali na kuisafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Cargo Granat.
Meli ya mizigo Natasha huko Ubelgiji.
Maersk liner.

Kuna meli za mizigo elfu nyingi zinazosafiri kwenye bahari, maziwa na mito mikubwa ya Dunia. Zinabeba sehemu kubwa ya bidhaa za biashara ya kimataifa. Meli za mizigo kwa kawaida hutengenezwa kwa kazi maalumu kama vile kubeba kontena, mizigo ya mchanganyiko, shehena za mafuta au gesi.

Siku hizi hutengenezwa kwa feleji na kusukumwa kwa injini za dizeli. Kuna pia majaribio ya kutumia nguvu ya upepo au umeme. Ziko kubwa na ndogo na kwa kawaid huwa na maisha ya kazi ya miaka 20 hadi 30 hadi kupumzishwa na kubomolewa tena.

Meli za mizigo za kisasa zinaweza kubeba mizigo mingi na mizito kama vile magari, mashine mbalimbali za kazi na kusafirisha kutoka bara moja kwenda bara jingine.

Meli hizi hutumia muda mrefu kufika sehemu husika kwani kuna muda meli hizi husumbuliwa na dhoruba za majini kama vile mawimbi, na muda mwingine meli hizi huhitaji kufanyiwa matengenezo ili ziweze kuendelea na safari zake.

Meli hizi zipo za aina nyingi, zipo zilizotengenezwa kwa ajili ya kusafirisha vyakula na matunda ambapo ndani huwa kuna majokofu kwa ajili ya kutunza vyakula na matunda hayo ili yasiharibike njiani kwani vyakula huhitaji uangalizi mzuri ili visiharibike.

Pia zipo meli za mizigo zilizotengenezwa kwa ajili ya kusafirisha mafuta kama petroli na dizeli, ambapo ndani ya meli hizi kuna matenki ya kubebea mafuta.

Meli huwa na mstari chini yake; mstari huo mara nyingi huwa wa rangi nyekundu au nyeusi, na mstari huu hautakiwi kuzama kabisa ndani ya maji kwani meli inaweza kuzama pale tu mstari huu utakapo zama wote ndani ya maji. Pia meli hizi hazitakiwi kutembea katika maji yenye kina kifupi kwani zinaweza kuzama.

Viungo vya Nje

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

  Freighter_travel travel guide kutoka Wikisafiri