Mfumo wa uongozaji kwa satelaiti

Mfumo wa uongozaji kwa satelaiti ni mfumo wa mitambo inayoruhusu kutambua kikamilifu mahali na mwelekeo.

Marudio (frequencies) ya mifumo mbalimbali ya uongozaji kwa satelaiti

Kipokeaji kinapokea ishara zinazotoka katika satelaiti. Satelaiti hurusha mfululizo ishara zenye habari juu ya wakati kamili kwenye satelaiti pamoja na majiranukta za satelaiti. Ishara za satelaiti nne zinatosha kutambua kwa umakini mahali pa kipokeaji kwa latitudo, longitudo na kimo.

Siku hizi simujanja na mitambo mingine huwa na sehemu ya kipokeaji kinachoweza kupata ishara za satelaiti.

Kuna mifumo za satelaiti zinazopatikana kote duniani, ambazo kwenye mwaka 2022 zilikuwa:

Mnamo mwaka 2022 GPS ilitumika zaidi kimataifa.

Nchi nyingine zimeanzisha mfumo kama huo ingawa hadi sasa satelaiti zao zinatosha kwa sehemu ya Dunia tu, mfano Uhindi[3] na Japani.

Mifumo hii ina satelaiti 24 hadi 30 ambazo zinazotosha ili angalau 4 zinaweza kupokelewa mahali popote duniani. Zinazunguka Dunia kwenye kimo cha kilomita 25,000 penye obiti ya mbali ambako wakati wa obiti unalingana na kasi ya Dunia ya kujizungusha na hivyo satelaiti hutazama muda wote sehemu hiyohiyo ya Dunia (geostationary orbit).

Marejeo

hariri
  1. "Galileo Initial Services". gsa.europa.eu. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "China's GPS rival Beidou is now fully operational after final satellite launched". cnn.com. Iliwekwa mnamo 2020-06-26.
  3. "Global Indian Navigation system on cards", The Hindu Business Line, 2010-05-14. (en)