Chati bega-jeupe
Chati bega-jeupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Muscicapidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Jenasi: Myrmecocichla
Cabanis, 1850
Spishi: M. nigra
(Vieillot, 1818)

Chati bega-jeupe (Myrmecocichla nigra) au mhozo mweusi ni ndege mwimbaji wa familia Muscicapidae (shore).

Maelezo

hariri

Ndege hawa ni wanono wenye mkia mfupi na wana ukubwa wa cm 15-16. Dume ni mweusi mwenye kidoa cheupe kwa bega la bawa. Jike na wachanga wana rangi ya kahawa nyeusi. Mara nyingi huonekana juu ya vichuguu. Hula wadudu na tunda madogo. Huimba wimbo wao wenyewe lakini mara nyingi huiga nyimbo za ndege wengine. Tago lao hujengwa kwa vitu vyororo kama nyasi, sufu, manyoya na nyuzinyuzi mwishoni kwa kishimo kilichochimbwa ndani ya kichuguu, dari ya shimo la muhanga au shimo lolote. Jike hutaga mayai 3-4.

Usambazaji

hariri

Spishi hii inatokea savana za Afrika chini ya Sahara katika nchi za Angola, Burundi, Gabon, Guinea, Guinea ya Ikweta, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Kameruni, Kenya, Liberia, Nigeria, Rwanda, Senegal, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia. Katika Afrika ya Mashariki wako wengi sana kwa Masai Mara na Serengeti. Kwa kadiri ya IUCN (Muungano wa Dunia wa Hifadhi) hakuna hangaiko kuhusu spishi hii.

Marejeo

hariri
  • Zimmerman, Dale A., Donald A. Turner, and David J. Pearson (1999). Birds of Kenya and Northern Tanzania. Princeton University Press, 198–199, 450. ISBN 0-691-01022-6.
  • Tanzaniabirds.net: Sooty chat
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chati Bega-jeupe kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.