Microsoft Corporation ni kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya kompyuta. [2] Neno Microsoft ni neno unganifu lilitokana na maneno ya Kiingereza "microcomputer" na "software".

Windows
Microsoft
IlipoanzishwaAlbuquerque, New Mexico (Aprili 4, 1975 (1975-04-04))[1]
Makao MakuuRedmond, Washington, Marekani
Mapato kabla ya riba na kodidecrease US$ 20.363 billion (2009)
Net incomedecrease US$ 14.569 billion (2009)
Total equityincrease US$ 39.558 billion (2009)
Tovutidjt5 Microsoft.com
Mti unaotunzwa na Microsoft karibu na ofisi ya Dell, Bangalore, India.

Kampuni ilianzishwa na William Henry Gates III (anayefahamika zaidi kama Bill Gates) na Paul Allen 04 Aprili 1977, ili kuendeleza na kuuza mifumo-ongozo rahisi kwa ajili ya kompyuta ndogo za Altair 8800. Kampuni hili liliinuka na kutawala soko la utengenezaji wa mifumo-ongozo ya kompyuta binafsi kupitia mfumo wake unaojulikana kama Microsoft- Disk Operating System (MS-DOS) katikati ya miaka ya 1980, ikifuatiwa na programu ya Microsoft Windows[3].

Makao makuu yako Redmond, Washington, Marekani.

Kampuni hii inaendeleza, kutengeneza, kutoa leseni, kusaidia na kuuza programu za kompyuta, vifaa vya umeme, kompyuta binafsi pamoja na huduma zihusianazo na hizo. Programu yake ya kompyuta ijulikanayo sana ni mfumo ongozo wa kompyuta wa Microsoft Windows, na programu nyingine kama vile, Microsoft Office, na Internet Explorer pamoja na Edge Web. Vifaa vyake maarufu ni vifaa michezo vya Xbox pamoja na mfumo wa kioomguso uitwao Microsoft Surface lineup kwa ajili ya kompyuta binafsi.

Kwa mwaka wa 2016, ndiyo kampuni kubwa duniani yenye kutengeneza programu za kompyuta kwa makusanyo ya jumla, na ni moja kati ya kampuni zenye thamani kubwa zaidi duniani. Microsoft ni kampuni iliyoko nafasi ya 31 katika orodha ya mwaka 2018 ya Fortune 500 ya mashirika makuu makubwa ya Marekani na mapato ya jumla.

Tanbihi hariri

  1. "Bill Gates: A timeline", news.bbc.co.uk, BBC News, 2006-06-15. Retrieved on 2008-08-18. 
  2. Microsoft Corporation Annual Report 2005 (doc). Microsoft. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba, 2005.
  3. Information for Students: Key Events In Microsoft History (doc). Microsoft Visitor Center Student Information. Iliwekwa mnamo 1 Oktoba 2005.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Microsoft kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.