Mijin anatajwa kati ya Wakristo wa kwanza kuuawa kwa ajili ya imani yake barani Afrika (180 hivi).

Ni kati ya wafiadini wa Madauros (karibu na M'Daourouch, leo nchini Algeria), pamoja na Namfamo, Sanami na Luchíta[1]. Majina mengine yanayotajwa pamoja ni: Adyuto, Aresto, Artifa, Besa, Datulo, Degno, Evasi, Felisi, Felisiani, Kresto, Kwarti, Kwinti, Lukania, Martiri, Mose, Museo, Onorato, Orato, Paulo, Pompini, Privati, Reduktula, Rogasiani, Rustiko, Salvatori, Saturnini, Setimini, Sesiliana, Seliani, Sidini, Simplisi, Sito, Teturo, Tino, Vikta, Viktorino, Vikturi na Vinsenti.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu kadiri ya barua ya Masimo wa Madaura kwa Augustino wa Hippo.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 18 Desemba[2][3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.