Mikoa ya Senegal
Mikoa ya Senegal ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini Senegal katika Afrika ya Magharibi. Senegal imegawanywa katika mikoa 14 (kwa Kifaransa: régions). Kila mkoa unasimamiwa na halmashauri yake (Conseil Régional) ambayo wajumbe wake wanachaguliwa na wananchi kwenye ngazi ya tarafa.
Ngazi ya pili ya ugatuzi ni wilaya (departements) 45, tarafa (arrondissements) 103 (ambazo hazina kazi ya kiutawala) na maeneo ya jumuiya za kieneo (collectivités locales) ambazo huchagua maafisa wa utawala.
Orodha ifuatayo inaonyesha mikoa ya Senegal pamoja na idadi ya wakazi kufuatana na sensa ya mwaka 2013.[1]
Mkoa | Makao makuu | Eneo (km²) |
Wakazi (sensa 2013) |
---|---|---|---|
Dakar | Dakar | 547 | 3,137,196 |
Ziguinchor | Ziguinchor | 7,352 | 549,151 |
Diourbel | Diourbel | 4,824 | 1,497,455 |
Saint-Louis | Saint-Louis | 19,241 | 908,942 |
Tambacounda | Tambacounda | 42,364 | 681,310 |
Kaolack | Kaolack | 5,357 | 960,875 |
Thiès | Thiès | 6,670 | 1,788,864 |
Louga | Louga | 24,889 | 874,193 |
Fatick | Fatick | 6,849 | 835,352 |
Kolda | Kolda | 13,771 | 714,392 |
Matam | Matam | 29,445 | 562,539 |
Kaffrine | Kaffrine | 11,262 | 566,992 |
Kédougou | Kédougou | 16,800 | 152,357 |
Sédhiou | Sédhiou | 7,341 | 452,944 |
Marejeo
hariri- ↑ Senegal: Administrative Division, tovuti ya Citypopulation.de, iliangaliwa Januari 2022