Mimi Mars
Marianne Namshali Mdee (maarufu kwa jina la kisanii kama Mimi Mars, Triple Threat au Chugga Queen alizaliwa Paris nchini Ufaransa, 21 Juni 1992) ni msanii wa Bongo Flava, R&B na Pop kutoka Tanzania[1][2][3][4]. Mimi Mars pia ni muigizaji, mshawishi (influencer), mshereheshaji na mtangazaji wa vipindi vya televisheni[5][6]. Anajulikana kwa sauti yake kwenye uimbaji na uchezaji (dansi).
Mimi Mars | |
---|---|
Amezaliwa | Juni 21 1992 |
Kazi yake |
|
Miaka ya kazi | 2017-mpaka sasa |
Studio | Mdee Music |
Tovuti | https://okaymusic.com/collections/mimi-mars |
Maisha ya awali
haririMimi Mars alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa akakulia Arusha, Tanzania. Amesoma shule ya msingi Arusha Modern School na sekondari St. Catherine’s Mountain View iliyopo jijini Nairobi, Kenya [7].
Ni mzaliwa wa mwisho kwenye familia yao, ndugu zake wengine wakiwa ni waimbaji wa nyimbo za Injili, Nancy Hebron ni mwanamuziki wa Pop Vanessa Mdee[8].
Alizaliwa kwenye familia ya wanamuziki, hivyo yeye na ndugu zake waliomtangulia walionyesha kupenda muziki tangu utotoni na walitumbuiza kwenye matukio mbalimbali ya kifamilia. Mwaka 2018 Mimi Mars alishirikiana na dada zake kutoa kibao kiitwacho “Beautiful Jesus” [9][10].
Kazi na muziki
haririAkiwa na umri wa miaka 11, Mimi Mars alishirikishwa kwenye tangazo la kampuni ya Tan Foam akiwa na baba yake. Inasemekana alianzia fani ya sanaa kwenye kutokea YouTube kabla ya kuingia rasmi kwenye muziki[11][12].
Mimi Mars ameanza rasmi muziki tarehe 22 Februari 2017 na kibao cha "shuga" ambacho kiliweza kushika chati za juu. Baadhi ya nyimbo zake ni "Niguse", "One Night" aliyomshirikisha mwanamuziki Kagwe Mungai, "Ringtone", "Mua", "Niache" na "Mdogo mdogo" aliyomshirikisha Nikki wa Pili. Nyimbo nyingine maarufu ni kama “Kodoo”, “Sitamani”, “Papara”, “Dedee” na “Down” aliyotoa kushirikiana na Quick Rocka. [13][14].
Pia, mwaka 2019 alishiriki Coke Studio [15]. Mwaka huo huo alishirikiana na shirika la kimataifa la watoto kwenye kampeni ya kuwalinda watoto na vijana ambapo alitoa kibao kiitwacho "Watoto tuwalinde"[16]
Pia anajishughulisha na kazi za sanaa ya uigizaji akishiriki kwenye tamthilia mbalimbali ikiwemo Jua kali na Jiya
Tazama pia
haririKazi za Nje ya Muziki
haririMbali na muziki, Mimi Mars ni mtangazaji wa televisheni na ameshiriki kwenye vipindi vya burudani na mitindo. Pia ni mjasiriamali mwenye chapa ya bidhaa za urembo na mitindo.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.capitalfm.co.ke/thesauce/tanzanian-songstress-mimi-mars-taking-over-kenya-with-her-latest-ep/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-07. Iliwekwa mnamo 2020-04-07.
- ↑ https://www.ippmedia.com/en/node/69589
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/Michezo/burudani/Mimi-Mars-kuwania-tuzo-za-filamu-Kenya/1597574-5338790-gab2t5/index.html
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/Michezo/burudani/Mimi-Mars-kuwania-tuzo-za-filamu-Kenya/1597574-5338790-gab2t5/index.html
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-07. Iliwekwa mnamo 2020-04-07.
- ↑ https://www.capitalfm.co.ke/thesauce/tanzanian-songstress-mimi-mars-taking-over-kenya-with-her-latest-ep/

- ↑ https://tanzania.un.org/en/29077-unicef-hand-over-children-young-peoples-agenda
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mimi Mars kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |