Bié (mkoa)
(Elekezwa kutoka Mkoa wa Bié)
Bié ni mkoa wa Angola wenye eneo la km² 70,314 na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya lakhi nane na milioni moja.
Makao makuu ya mkoa yako mjini Kuito (Cuito).
Hali ya hewa haina joto kali kutokana na milima na mvua ya mara kwa mara. Hayo yote huwezesha kilimo cha mahindi, karanga, miwa, kahawa na mpunga.
Mkoa ni sehemu ya Nyanda za Juu za Bie. Kuna njia ya reli kati ya mkoa na pwani.
Miji mikubwa zaidi mkoani ni:
- Kuito- wakazi 114 791
- Camacupa- wakazi 19 347
- Catabola- wakazi 19 281
- Catumbela- wakazi 17 369
- Chisamba- wakazi 7 755
Nyumba ya mwenyekiti wa chama cha UNITA Isaias Samakuva iko mkoani kwenye mji wa Kunji.
Viungo vya Nje
hariri- US government statistics from 1988
- angola.org.uk Archived 15 Juni 2007 at the Wayback Machine.
Bengo | Benguela | Bié | Cuando Cubango | Cuanza Kaskazini | Cuanza Kusini | Cunene | Huambo | Huíla | Kabinda | Luanda | Lunda Kaskazini | Lunda Kusini | Malanje | Moxico | Namibe | Uíge | Zaire |
Makala hii kuhusu maeneo ya Angola bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bié (mkoa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |