Mpasuaji ni daktari wa tiba ambaye hufanya shughuli za upasuaji katika viungo mbalimbali vya binadamu.

Sanamu ya daktari Mhindi wa kale, Sushruta, mpasuaji wa kwanza katika kumbukumbu za dunia, ambaye huchukuliwa kama 'Baba wa Utabibu wa Upasuaji' na mmoja wa waanzilishi wa Upasuaji wa plastiki ambao kazi yake kubwa ni kurekebisha viungo vya mwili na hata kwa urembo hasa miaka ya karibuni.

Pia kuna upasuaji katika utabibu wa meno na utabibu wa mifugo.

Historia

hariri
 
Al-Zahrawi, aliyeishi Nyakati za dhahabu za Kiislamu (Islamic Golden Age), ni daktari anayechukuliwa kuwa '"Baba wa Upasuaji wa Kisasa".

Mtu wa kwanza kuwekwa kwenye kumbukumbu kama daktari mpasuaji ni Sushruta aliyeishi karne ya 6. Yeye alifanya upasuaji wa plastiki peke yake[1]. Hati yake muhimu kabisa: Suśruta-saṃhitā ni moja ya hati muhimu zaidi za kale zilizoko kuhusu matibabu na huchukuliwa kama nakala msingi ya Ayurveda na upasuaji. Hati hii huongea kuhusu mambo yote ya matibabu ya kijumla, lakini mtafsiri G. D. Singhal alimwita Suśruta "baba wa upasuaji" kwa sababu ya usahihi usio wa kawaida na wa kina uliomo katika hati hizo.[2]

Upasuaji ulipuuziwa kijumla hadi "Nyakati za dhahabu za Kiislamu" ambapo mpasuaji Al-Zahrawi (936-1013) alistawisha matibabu ya upasuaji. Yeye huchukuliwa kama mpasuaji mkuu zaidi wa kale aliyetoka Ulimwengu wa Kiislamu.[3] Mchango wake mkubwa kwa matibabu ni Kitab al-Tasrif, kamusi elezo ya matibabu yenye juzuu thelathini.[4] Yeye alikuwa daktari wa kwanza kuelezea hali ya mimba kutoka chungu cha mtoto, na daktari wa kwanza kutambua asili ya kijenetikia ya haemophilia.

Michango yake kwenye tasnia ya taratibu za upasuaji na zana ilichangia kwa kiasi kikubwa upasuaji lakini haikuwa hadi karne ya 19 ambapo upasuaji ulichukuliwa kama tasnia kivyake katika matibabu huko Ulaya na ulimwengu wa Magharibi.[5]

Katika Ulaya, upasuaji mara nyingi ulihusishwa na vinyozi-wapasuaji waliotumia zana zao za kunyoa nywele kufanya upasuaji, mara nyingi katika vita na pia kwa wadhamini wao wa kifalme.

Pamoja na maendeleo katika dawa na tiba, fani ya vinyozi na wapasuaji zilitengana; kwa karne ya 19 vinyozi-wapasuaji walikuwa karibu kutoweka, na wapasuaji walikuwa madaktari waliohitimu ambao walishikilia upasuaji pekee. 

Wapasuaji waanzilishi

hariri
 
Mpasuaji Mrusi Nikolay Pirogov - mwanzilishi wa upasuaji wa vitani
 
Victor Horsley mwanzilishi wa upasuaji wa uti wa mgongo na seli za hisia

Marejeo

hariri
  1. Ira D. Papel, John Frodel, Facial Plastic and Reconstructive Surgery
  2. Singhal, G. D. (1972). Diagnostic considerations in ancient Indian surgery: (based on Nidāna-Sthāna of Suśruta Saṁhitā). Varanasi: Singhal Publications.
  3. Ahmad, Z. (St Thomas' Hospital) (2007), "Al-Zahrawi - The Father of Surgery", ANZ Journal of Surgery, 77 (Suppl. 1): A83, doi:10.1111/j.1445-2197.2007.04130_8.x
  4. al-Zahrāwī, Abū al-Qāsim Khalaf ibn ʻAbbās; Studies, Gustave E. von Grunebaum Center for Near Eastern (1973). Albucasis on surgery and instruments. University of California Press. ISBN 978-0-520-01532-6. Iliwekwa mnamo 16 Mei 2011.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Cosman, Madeleine Pelner; Jones, Linda Gale (2008). Handbook to Life in the Medieval World. Handbook to Life Series. Juz. la 2. Infobase Publishing. ku. 528–530. ISBN 0-8160-4887-8.
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mpasuaji kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.