Msaada wa Masomo ya Lugha za Kipeo
Msaada wa Masomo ya Lugha za Kipeo (“Critical Language Scholarship” au “CLS” kwa Kiingereza) ni programu kwa wanafunzi Wamarekani ili kujifunza lugha zinazotoka nchi nyingi tofauti duniani ambazo ni muhimu sana kwa ushirikiano na usalama wa Marekani. Wanafunzi wanasoma lugha na wanajifunza kuhusu utamaduni wa eneo ambapo watu wanasema lugha hii.[1]
Wakati wa Programu
haririWanafunzi ambao wanapata msaada wa masomo ya lugha za kipea watasafiri nchi ambapo watu wanasema lugha hii kwa wiki nane au wiki kumi.[1] Wanafunzi watakwenda darasa la lugha kwa masaa kumi na tano au zaidi kila wiki; kwa hiyo, watajifunza masomo sawa na mwaka moja wa kusoma katika Chuo Kikuu. Pia, nje ya darasa, wanafunzi wataweza kuzungumza na mbia wa mazungumzo na wataweza kutalii nchi na utamaduni. Serikali ya Marekani inalipia masomo, vitabu, usafiri mpaka na toka nchi ya mwenyeji, nyumba, na chakula kwa wanafunzi wa Msaada wa Masomo ya Lugha za Kipeo.[2]
Lugha za Kipeo
hariri-
Bendera ya China (Kichina)
-
Bendera ya Japan (Kijapani)
-
Bendera ya India (Kihindi)
-
Bendera ya Ureno (Kireno)
-
Bendera ya Tanzania (Kiswahili)
Wanafunzi wanaweza kusoma lugha moja ya lugha kumi na tano:
- Kiarabu*
- Kiazerbaijani
- Kichina*
- Kihindi
- Kiindonesia
- Kijapani**
- Kikorea
- Kiajemi
- Kireno
- Kirusi*
- Kiswahili
- Kituruki
*Wanafunzi wanahitaji wamesoma lugha hii kwa mwaka mmoja au zaidi kabla ya kufanya CLS
**Wanafunzi wanahitaji wamesoma lugha hii kwa miaka miwili au zaidi kabla ya kufanya CLS[3]
Lugha hizi ni lugha ambazo nchi ya Marekani anasema ni muhimu sana kwa nchi kuelewa na kuungana na nchi nyingine duniani.[1] Pia, lugha hizi hazifundishwi mara nyingi katika shule nyingi Marekani.[4]
Programu Katika Afrika Mashariki - Kiswahili
haririLugha moja wapo unaweza kusoma katika Msaada wa Masomo ya Lugha za Kipeo ni Kiswahili, lugha muhimu sana Afrika Mashariki. Washindi wa msaada wa masomo kusoma Kiswahili wanasoma MS-TCDC katika mji wa Arusha, nchi ya Tanzania.[5] Kila mwaka, takriban wanafunzi ishirini wanapata msaada wa masomo huu ili kusoma Kiswahili. Angalia chini kuona wanafunzi wangapi walishinda msaada wa masomo huu kwa miaka nane iliopita:[6]
Mwaka | Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza | Wanafunzi wa Shahada ya Pili au Tatu | Wanafunzi Jumla |
2023 | 18 | 7 | 25 |
2022 | 18 | 14 | 32 |
2021 | 22 | 7 | 29 |
2020 | 10 | 3 | 13 |
2019 | 18 | 10 | 28 |
2018 | 23 | 4 | 27 |
2017 | 17 | 10 | 27 |
2016 | 17 | 6 | 23 |
Wahitimu wa Programu
haririBaada ya kufanya Msaada wa Masomo ya Lugha za Kipeo, wahitimu wa programu wameweza kusema lugha ambayo walisoma nzuri zaidi ya kabla ya kufanya programu. Hasa wanafunzi ambao walianza kuweza kusema lugha kidogo tu wanaendelezea sana.[7] Asilimia tisini na nane wa wahitimu walitumia lugha waliyosoma kwa programu ya CLS mwaka uliofuata mwaka waliofanya programu ya CLS.[8] Zaidi ya lugha tu, wahitimu wa CLS wanasema kwamba walijifunza ustadi wa mawasiliano kati ya utamaduni tofauti ambao umewasaidia kupata kazi.[9]
Msaada ya Masomo za Lugha Nyingine
haririKuna programu nyingi zaidi kama Msaada ya Masomo ya Lugha za Kipeo ambazo zinalipiwa na serikali ya Marekani kwa wanafunzi ambao wanataka kusoma lugha au utamaduni tofauti. Hizi ni programu chache:[10]
- Programu ya Msaada ya Masomo ya Mataifa ya Benjamin A. Gilman
- Programu ya Mwanafunzi Mmarekani ya Fulbright
- Tunzo la Boren kwa Kusoma kwa Mataifa
- Mpango GO
- Uanazuoni wa Masomo wa Lugha na Maeneo Mageni
Tanbihi
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Homepage". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "CLS Program". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Languages List". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Find Programs". exchanges.state.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Swahili". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Participants". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Language Learning Outcomes". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Long-Term Impact". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "Impact". Critical Language Scholarship Program (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
- ↑ "For U.S. College and University Students". USA StudyAbroad (kwa Kiingereza). 2015-11-05. Iliwekwa mnamo 2024-04-24.