Msitu wa Mau

eneo la misitu katika Bonde la Ufa la Kenya. Ni msitu mkubwa zaidi wa asili wa montane katika Afrika ya Mashariki.

Msitu wa Mau ni msitu tata katika Bonde la Ufa nchini Kenya. Ni msitu asili wa milimani ulio mkubwa zaidi katika Afrika Mashariki. Msitu tata wa Mau una eneo wa hektari 273300.

Maeneo ya misitu yana baadhi ya viwango vya juu kabisa ya mvua nchini Kenya [1] Misitu ya Mau ni eneo kubwa ya vyanzo vya maji nchini Kenya [2] Mito kadhaa huanza kutoka misitu hii, ikiwemo mto Ewaso Ng'iro (kusini), mto Sondu, Mto Mara na Mto Njoro. Mito hiyo hulisha Ziwa Viktoria, Ziwa Nakuru na Ziwa Natron [1] Miteremko ya mashariki ya bonde la Mau imejazwa msitu wa Mau [1]

Mazingira hariri

Miti asilia katika msitu wa Mau ni pamoja na Pouteria adolfi-friedericii, Strombosia scheffleri, Polyscias kikuyuensis, Olea capensis, Prunus africana, gummifera na Albizia Podocarpus latifolius[1]

Ndege wanaopatikana katika eneo hilo ni pamoja na Tauraco hartlaubi, Cisticola hunteri na Francolinus jacksoni. [1]

Uharibifu hariri

Katika miaka ya jadi misitu hii ilikuwa ikikaliwa na jamii ya Ogiek ,ambao maisha yao ya kuwinda na kukusanya ni endelevu [1] Hata hivyo, kutokana na watu kutoka makabila mengine kuhamia msitu huo, sehemu ya eneo la msitu imekatwa kwa ajili ya makazi. [8]

Katika mwaka wa 2008, uzinduzi wa mradi wa nguvu za umeme ya Sondu-Miriu Hydro uliahirishwa kutokana na kiwango cha chini cha maji, ambao ulisemekana ulitokana na uharibifu katika msitu wa Mau.

Uhamisho kutoka msitu wa Mau hariri

Katika msimu wa joto wa 2008 kulikuwa na mvutano wa kisiasa kuhusu swala la makazi ya watu, ambayo yalikuwa yametengwa katika uongozi wa KANU katika miaka ya 80 na 90. Baadhi ya walowezi ni wanasiasa mashuhuri, kama Franklin Bett na Zakayo Cheruiyot. Katika mwaka wa 2004 Paul Ndung'u alitoa "Ndungu Report", ambayo ilitaja kugawa ardhi hizi, kuwa haramu na ilipendekeza ugawavi huu utupiliwe mbali.[2] Baadhi ya uhamisho ulitekelezwa kati ya mwaka wa 2004 na 2006, bila ya mfuko wa makazi [3]

Mnamo 15 Julai 2008, Waziri Mkuu Raila Odinga alitoa amri kwamba uhamisho utekelezwe kabla ya mwezi wa Oktoba 2008, ili kulinda misitu kutokana na uharibifu [4] Amri hii imepingwa na baadhi ya wanasiasa wa eneo la Bonde la Ufa, wakiongozwa na Isaac Ruto. Baadhi ya wanasiasa, wakiongozwa na waziri wa kilimo William Ruto, walipendekeza kwamba iwapo uhamisho utatekelezwa, serikali inapaswa kuwatengea ardhi wanaohamishwa mahali pengine [2]

Uhamisho ulianza Novemba 2009. Pia baadhi ya watu mashuhuri wanaelekea kupoteza ardhi yao, wakiwemo pamoja na familia ya rais wa zamani Daniel arap Moi [5]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named IBA
  2. 2.0 2.1 2.2 Daily Nation, 22 Julai 2008: Tamaa kutatiza msitu wa Mau
  3. Amnesty International: Kenya haina pahali pa kuenda: Nakala kuhusu kuhamishwa kwa lazima kutoka msitu wa Mau,Mei 2007
  4. Capital News, 15 Julai 2008: [1] Archived 22 Julai 2011 at the Wayback Machine. Mkutano wa Raila yapitisha uhamishaji kutoka Mau
  5. Daily Nation, 28 Novemba 2009:Majina mashuhuri na maaskari kufuata katika hamisho

Viungo vya nje hariri